Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-NELSON MANDELA

Misururu ya waombolezaji yaendelea kushuhudiwa Afrika Kusini katika siku ya mwisho kumuaga Hayati Nelson Mandela

Wananchi wa Afrika Kusini wamekesha katika misururu usiku kucha wakisubiri kuuaga mwili wa Rais wa kwanza mzalendo wa Taifa hilo Nelson Mandela aliyefariki dunia siku ya alhamisi juma lililopita jijini Johannesburg. Leo ijumaa ni siku ya mwisho kwa mwili wa kiongozi huyo kuagwa na wananchi kabla ya kupelekwa kijijini kwake Qunu ambako mazishi yatafanyika jumapili tarehe 15 Desemba.

REUTERS/Kevin Coombs
Matangazo ya kibiashara

Idadi kubwa ya watu wamejitokeza kuuaga mwili wa kiongozi huyo katika siku tatu zilizopangwa, na serikali imeonya kuwa kutokana na umati kuwa mkubwa zaidi huenda wengine wakakosa nafasi hiyo.

Watu wengi hawakurejea makwao na wamelala nje ya eneo lililofadhiwa mwili wa Mandela ili waweze kuwahi nafasi ya mwisho hii leo.

Mwili wa Mandela utawasili katika kijiji cha Qunu kesho jumamosi, na watu takribani watu 5,000 toka mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhudhuria mazishi yake siku ya jumapili.

Lakini wakazi wa kijiji hicho wanalalamika kwa kutopewa nafasi ya kutoa heshima za mwisho mara mwili wa kiongozi huyo utakapowasili.

Wanahabari wapatao 3,000 tayari wamewasili kijijini Qunu ambako maandalizi ya mapokezi ya mwili wa Mandela yanaendelea.

Mazishi hayo yatafanyika kwa mujibu wa tamaduni za Jamii ya Xhosa yakishuhudiwa na wanaume wa ukoo wa Mandela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.