Pata taarifa kuu
KUWAIT

Mkutano wa mataifa ya kiarabu wafunguliwa huku mzozo wa Syria ukitajwa

Kiongozi wa Kuwait Emir Sheikh Sabah al-Ahmad Al-Sabah amefungua mkutano wa wakuu wa mataifa ya kiarabu Jumanne kwa kutoa wito wa kumalizika kwa machafuko nchini Syria. 

Rais wa Kuwait Sheikh Sabah al-Ahmad Al-Sabah
Rais wa Kuwait Sheikh Sabah al-Ahmad Al-Sabah www.da.gov.kw
Matangazo ya kibiashara

Sheikh Sabah, amelaumu umoja wa mataifa kwa kushindwa kuumaliza mzozo wa syria ambao umedumu kwa miezi 33 sasa.

Mkutano huo wa kilele unafuatia malumbano nadra ya umma kati ya kiongozi wa kanda ya Saudi Arabia na Oman kuhusu pendekezo la Riyadh la kuipandisha GCC kuwa muungano, miaka 32 baada ya kuanzishwa kwake.

Waziri wa mambo ya nje wa Omani Yussef bin Alawi alitishia kwamba Muscat itajiondoa kwenye muungano huo unaotetereka ikiwa muungano utatangazwa, wakati Saudi Arabia ikiungwa mkono kwa dhati na Bahrain ilisisitiza kuwa ni wakati wa kusonga mbele.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.