Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Homa ya matokeo ya uchaguzi yapanda Zimbabwe wakati ambapo kura zinahesabiwa

Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Zimbabwe baada ya wananchi kupiga kura jumatatu kuchagua rais, wabunge na wawakilishi kwenye uchaguzi uliokuwa wa kihistoria na wa kwanza kufanyika chini ya katiba mpya.

Tayari zoezi la kuhesabu kura limeanza nchini Zimbabwe,ambapo mahasimu wa kisiasa Robert Mugabe na Morgan Tsvangirai wakitupiwa macho kwa karibu.
Tayari zoezi la kuhesabu kura limeanza nchini Zimbabwe,ambapo mahasimu wa kisiasa Robert Mugabe na Morgan Tsvangirai wakitupiwa macho kwa karibu. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wasimamizi wa uchaguzi mjini Harare Katika jitihada za kukamilisha zoezi la upigaji kura baadhi ya vituo vya kupigia kura vililazimika kusalia wazi hadi usiku ili kuhakikisha wananchi waliojitokeza katika misururu kupiga kura wamekamilisha haki yao.

Kiongozi wa Tume ya uchaguzi nchini humo Ritha Makarau amewaambia waandishi wa habari kuwa zoezi la kuhesabu kura lilianza usiku wa jumatano kama ilivyopangwa na utaratibu umefanyika ili kuhakikish raia ambao hawakuweza kupiga kura wanapatiwa fursa ya kupiga kura.

Zoezi la upigaji kura lilikabiliwa na changamoto chache kama alivyobainisha Makarau ikiwemo kuendeshwa kwa kasi ndogo na muda wa kukagua vithibitisho vya mpiga kura.

Vilevile Makarau alibainisha kuwa Tume ya taifa ya uchaguzi ya Zimbabwe imepokea hati za kughushi takribani 20 huko mjini Harare na tukio hilo linafanyiwa uchunguzi.

Uchaguzi huu unatajwa kumpa changamoto kubwa raisi mkongwe Robert Gabriel Mugabe ambaye amekuwepo madarakani kwa zaidi ya miaka thelethini ambapo sasa Macho na masikio ya Ulimwengu yanaelekezwa Zimbabwe kujua nini kitaamuliwa kupitia kura za raia kati ya mabadiliko au mwendelezo wa utawala.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.