Pata taarifa kuu
SIASA-UFISADI

Rais wa Vietnam Vo Van Thuong atangaza kujiuzulu

Rais wa Vietnam Vo Van Thuong amewasilisha barua yake ya kujiuzulu siku ya Jumatano, baada ya mwaka mmoja tu madarakani, vimetangaza vyombo vya habari vya serikali ya nchi hii ya kikomunisti, inayotangaza kuanzisha operesheni kubwa ya kupambana na rushwa. 

Vo Van Thuong alikuwa rais mnamo Machi 2, 2023, baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake, Nguyen Xuan Phuc, tukio lisilo la kawaida huko Vietnam.
Vo Van Thuong alikuwa rais mnamo Machi 2, 2023, baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake, Nguyen Xuan Phuc, tukio lisilo la kawaida huko Vietnam. AP - Nhan Huu Sang
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika la habari la serikali la VNA, rais ametangaza kuwa ana hatia ya "ukiukaji na mapungufu", na kujiuzulu kwake kumekubaliwa na kamati kuu ya Chama tawala cha Kikomunisti.

Tangazo hilo la kustaajabisha la kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 53 linakuja wakati Vietnam ikikumbwa na msukosuko mkubwa wa kisiasa, huku mtangulizi wake pia akitimuliwa mamlakani kama sehemu ya operesheni ya kupambana na ufisadi ambayo ilishuhudia mawaziri kadhaa wakifukuzwa kazi na viongozi wa makampuni ya serikali wakifikishwa mahakamani kwa ulaghai na ufisadi.

Vo Van Thuong alikiuka "kanuni" ambazo hazijabainishwa, na alishindwa kutoa mfano kama mkuu wa nchi, shirika la habari la serikali la VNA limeripoti. "Ukiukaji na mapungufu ya Comrade Vo Van Thuong yalionekana vibaya na raia, na kuathiri sifa ya Chama, serikali na yeye mwenyewe," VNA imeongeza. "Akijua kikamilifu wajibu wake kwa Chama, Serikali na raia wake, ameamua kujiuzulu kwa majukumu aliyokabidhiwa."

Vo Van Thuong alikuwa rais mnamo Machi 2, 2023, baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake, Nguyen Xuan Phuc, tukio lisilo la kawaida huko Vietnam, ambapo utulivu unapewa kipao mbele na mabadiliko ya kisiasa kupangwa kwa uangalifu. Kabla ya Nguyen Xuaen Phuc, ni rais mmoja tu wa Vietnam aliyejiuzulu, kwa sababu za kiafya. Ingawa rais ndiye mkuu wa nchi, kiongozi shupavu wa utawala huo ni katibu mkuu wa chama, Nguyen Phu Trong, anayechukuliwa kuwa mwanzilishi wa kampeni ya kupambana na ufisadi, ambaye ni maarufu nchini Vitenam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.