Pata taarifa kuu

Kifo cha Navalny: Mama wa mpinzani anaishutumu Urusi kwa kutaka kumzika mwnae kwa siri

Siku sita baada ya kifo cha mtoto wake na baada ya kutoa wito moja kwa moja kwa Vladimir Putin, mama wa mpinzani wa Urusi Alexei Navalny amesema ameweza kuona mwili wa mwanae na cheti cha kifo chake. Lakini katika video mpya, anawashutumu wale walio mamlakani kwa kumdhaliliha kuhusu mazingira ya mazishi ya mwanawe.

Mama wa mpinzani wa Urusi Alexei Navalny, Lyudmila Navalnaya, anazungumza kwenye video mpya na anadai kuwa aliweza kuona mwili wa mtoto wake mnamo Februari 22, 2024.
Mama wa mpinzani wa Urusi Alexei Navalny, Lyudmila Navalnaya, anazungumza kwenye video mpya na anadai kuwa aliweza kuona mwili wa mtoto wake mnamo Februari 22, 2024. via REUTERS - ALEXEI NAVALNY YOUTUBE CHANNEL
Matangazo ya kibiashara

Mazishi kufanyika kwa usiri mkubwa. Mamake Alexeï Navalny, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 47 siku sita zilizopita, amehakikisha siku ya Alhamisi kwamba ameweza kuuona mwili wa mtoto wake, baada ya siku kadhaa za kusubiri. Lakini katika video iliyotangazwa na timu ya mpinzani kwenye YouTube, Lyoudmila Navalnaïa ameshutumu "udhalilishaji" aliopata kutoka kwa mamlaka ya Urusi kutaka kumzika mwanawe kwa siri.

  “Wanataka kila kitu kifanywe kwa siri, bila sherehe, wanataka kunipeleka kwenye kaburini, karibu na kaburi mbichi, na kuniambia: 'Huyu mwanao amelala.' Sikubaliani na hii, "amesema Lyudmila Navalnaya. Kwa undani mama wa marehemu alidokeza kuwa alipelekwa chumba cha maiti na kuweza kuona mwili wa mwanae. Pia anasema yuko Salekhard, mji mkuu wa wilaya ya Yamalo-Nenetsia, eneo la Kaskazini ya Mbali ambapo Alexeï Navalny alifariki kizuizini mnamo Februari 16.

“Naomba mwili wa mwanangu urudishwe kwangu mara moja”

Kulingana na mama yake, wachunguzi tayari wamegundua sababu ya kifo, "na hati zote za kisheria na za matibabu ziko tayari." "Ilibidi nisaini cheti cha matibabu," ameongeza: kulingana na timu ya mpinzani, sababu ya kifo imetajwa kama ya "asili".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.