Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Putin kugombea kwenye kiti cha urais kama mgombea huru

Vladimir Putin atagombea tena katika uchaguzi wa urais kama mgombea huru, shirika la habari la RIA linaloungwa mkono na serikali limesema siku ya Jumamosi, likiwanukuu wabunge wawili wakuu wanaounga mkono Kremlin.

Bwana Putin alitoa shukrani zake kwa wajumbe wa vyama vya bunge wanaounga mkono "operesheni maalum ya kijeshi" nchini Ukraine, akisisitiza kujitolea kwao kwa Urusi na msaada wao kwa wanajeshi na familia zao.
Bwana Putin alitoa shukrani zake kwa wajumbe wa vyama vya bunge wanaounga mkono "operesheni maalum ya kijeshi" nchini Ukraine, akisisitiza kujitolea kwao kwa Urusi na msaada wao kwa wanajeshi na familia zao. REUTERS/Alexei Nikolsky/RIA Novost
Matangazo ya kibiashara

Akiwa madarakani kama rais au waziri mkuu kwa zaidi ya miongo miwili, Vladimir Putin ametangaza kuwa atawania muhula mwingine wa miaka sita mwezi Machi mwaka ujao, katika uchaguzi anaotarajiwa kuushinda.

Hatagombea kama mgombea wa chama tawala cha United Russia (UR), ingawa anaungwa mkono kikamilifu, lakini kama mgombea huru, Andrei Turchak, afisa mkuu wa chama, alinukuliwa na shirika la habari la RIA.

Sergei Mironov, afisa wa chama cha Just Russia, anayemuunga mkono Vladimir Putin, pia ameliambia shirika la habari la RIA kwamba rais atagombea kama mtu huru na kwamba saini zitakusanywa kwa niaba yake.

Vladimir Putin, mwenye umri wa miaka 71, anasema uchaguzi huu ni wa kawaida. Akiungwa mkono na serikali, vyombo vya habari vya umma na kutokuwepo kwa upinzani kwa maoni ya umma, ushindi wake unazingatiwa.

Wafuasi wake wasema kuwa alirejesha utulivu, sifa ya kitaifa na baadhi ya ushawishi ambao Urusi ilipoteza baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti. Pia wanahalalisha vita yake nchini Ukraine, ambayo anaiita "operesheni maalum ya kijeshi".

Ukandamizaji wa miaka mingi wa wapinzani na wakosoaji, ulioimarishwa na sheria mpya zinazoenea juu ya "habari za uwongo" na "kudharau jeshi," umesababisha vifungo virefu au kulazimishwa kutoroka nje ya nchi kwa wapinzani. Nafasi za wapinzani zimepungua polepole.

"Uingiliaji wowote wa kigeni utakandamizwa vikali"

Siku ya Ijumaa Vladimir Putin alitoa onyo dhidi ya "uingiliaji wowote wa kigeni" katika kampeni ya urais iliyopangwa mwezi wa Machi 2024 nchini Urusi, muktadha ulioangaziwa na mzozo wa Ukraine na ukandamizaji wa wapinzani wote.

Wakati wa mkutano wa televisheni na viongozi wa chama waliopo Duma, ikulu ndogo ya Bunge, rais anayegombea tena uchaguzi alisema:

“Uingiliaji wowote wa mambo ya ndani ya Urusi utaadhibiwa vikali kwa mujibu wa sheria za Urusi. "

Alisisitiza: “Tunatetea uhuru wa raia wetu, mamlaka yao na haki yao ya kuchagua mustakabali wao. Raia wa Urusi ndio chanzo pekee cha nguvu katika nchi yetu.

Bwana Putin alitoa shukrani zake kwa wajumbe wa vyama vya bunge wanaounga mkono "operesheni maalum ya kijeshi" nchini Ukraine, akisisitiza kujitolea kwao kwa Urusi na msaada wao kwa wanajeshi na familia zao.

Pia alitaja ongezeko kubwa la idadi ya askari wa Ukraine waliokamatwa katika siku za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.