Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Urusi yajiondoa katika mkataba wa kupiga marufuku majaribio ya nyuklia

Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Alhamisi ametia saini sheria ya kubatilisha uidhinishaji wa Mkataba wa Marufuku ya Majaribio ya Nyuklia (CTBT), dhidi ya hali ya mzozo nchini Ukraine na mgogoro na nchi za Magharibi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametia saini sheria ya kubatilisha uidhinishaji wa Mkataba wa Marufuku ya Majaribio ya Nyuklia (CTBT).
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametia saini sheria ya kubatilisha uidhinishaji wa Mkataba wa Marufuku ya Majaribio ya Nyuklia (CTBT). AFP - MIKHAIL METZEL
Matangazo ya kibiashara

Mkataba wa Kupiga Marufuku ya Majaribio ya Kinyuklia ulifunguliwa ili kutiwa saini mwaka wa 1996, lakini haukuanza kutumika kwa sababu haukuidhinishwa na idadi ya kutosha ya mataifa, kati ya nchi 44 zilizoshikilia mitambo ya nyuklia wakati wa kuundwa kwake.

Hati hiyo iliidhinishwa na Bunge la Seneti la Urusi mwishoni mwa mwezi wa Oktoba.

Mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba, Vladimir Putin alitangaza kuwa nchi yake inaweza kubatilisha uidhinishaji wa CTBT kwa kujibu Marekani ambayo haikuidhinisha kamwe. "Siko tayari kusema ikiwa tunapaswa kuanza tena majaribio au la," aliongeza, huku akipongeza maendeleo ya makombora mapya yenye uwezo wa juu ambayo yanaweza kubeba vichwa vya nyuklia.

"Majibu kwa mtazamo wa kuchukiza wa Marekani"

Tangu kuanza kwa mzozo nchini Ukraine mnamo mwezi wa Februari 2022, rais wa Urusi alito maneneo makali kuhusu utumiaji wa silaha za nyuklia, akituma silaha za nyuklia huko Belarusi, mshirika wake wa karibu, wakati wa kiangazi mnamo mwaka 2023. Sheria ya kubatilisha uidhinishaji wa Mkataba wa Marufuku ya Majaribio ya Nyuklia ilipitishwa kwanza na Β barazala la Wawakilishi (Duma), kabla ya kupitishwa kwa kauli moja na Bunge la Seneti mwishoni mwa mwezi wa Oktoba.

Spika wa Duma Vyacheslav Volodin aliita kura hiyo "jibu kwa mtazamo wa kuchukiza wa Marekani juu ya majukumu yake kuhusu kudumisha usalama wa ulimwengu." Mwishoni mwa mwezi Oktoba, Urusi pia ilifanya majaribio ya kurusha makombora ya balestiki kwa lengo la kuandaa vikosi vyake kwa "mashambulizi makubwa ya nyuklia" ya kujibu.

Β Mnamo Februari, Urusi pia ilisitisha ushiriki wake katika mkataba wa kutokomeza silaha za nyuklia wa New Start uliotiwa saini na Marekani mnamo 2010, makubaliano ya mwisho ya nchi mbili yanayounganisha Warusi na Wamarekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.