Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Putin ziarani nchini China kukutana na "rafiki yake kipenzi" Xi Jinping

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasili Beijing siku ya Jumanne, ambako anatazamiwa kukutana na mwenzake na "rafiki mpendwa" Xi Jinping, katika hafla ya mkutano mkubwa wa kilele wa pande nyingi ambao kwa kiasi fulani unapaswa kugubikwa na mzozo uliopo kati ya Israel na Hamas.

China inapendelea "suluhisho la amani" la mzozo wa Ukraine, kiongozi wa China Xi Jinping alimwambia rais wa Urusi Vladimir Putin, huku Beijing ikitaka kujiimarisha kama mpatanishi kati ya Moscow na Kiev.
China inapendelea "suluhisho la amani" la mzozo wa Ukraine, kiongozi wa China Xi Jinping alimwambia rais wa Urusi Vladimir Putin, huku Beijing ikitaka kujiimarisha kama mpatanishi kati ya Moscow na Kiev. AFP - GRIGORY SYSOYEV
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo alishuka kwenye ndege yake, ambayo ilitua muda mfupi kabla ya 9:30 asubuhi (sawa na 01:30 usiku saa za kimataifa) katika mji mkuu wa China, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

China itakuwa mwenyeji hadi Jumatano wawakilishi wa baadhi ya nchi 130 kwa ajili ya kongamano la "Njia Mpya za Hariri" (mradi ambao pia unaitwa "Ukanda na Barabara"), tukio kubwa la kidiplomasia ambalo linapaswa kusaidia kuimarisha hadhi yake ya kimataifa.

Mgeni mashuhuri, Vladimir Putin anafanya safari yake ya kwanza kwa nchi yenye nguvu kubwa duniani tangu uvamizi wa Ukraine mnamo Februari 2022, ambao ulisababisha Urusi kutengwa na mataifa mengine.

"Tarehe 18 Oktoba 2023 huko Beijing, kando ya Kongamano la tatu la Kimataifa la Belt and Road, mazungumzo yatafanyika kati ya rais wa Shirikisho la Urusi Vladimir Putin na rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping," imetangaza Moscow.

- Kupanda kwa Beijing juu ya Moscow -

Wawili hao "watajadili kwa njia ya kirafiki na ya wazi (...) matatizo ya dharura ya ushirikiano wa kivitendo baina ya nchi mbili na ajenda ya kimataifa", ameeleza mshauri wa kidiplomasia wa Kremlin, Yuri Ushakov.

Mwezi Machi mwaka huu, Vladimir Putin alimpokea Xi Jinping na walionyesha uelewa wao, wakitetea uimarishwaji wa ushirikiano wa kiuchumi na kijeshi ili kukabiliana na kile wanachowasilisha kama utawala wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.