Pata taarifa kuu

China: Xi Jinping athibitisha tena kipaumbele kwa 'utulivu wa kijamii' Xinjiang

Hakuna swali la kubadilisha sera katika jimbo la Xinjiang. Rais Xi Jinping wa China alithibitisha hayo Jumamosi Agosti 26 katika mji mkuu wa eneo linalojitawa la Uyghur magharibi mwa China. Hotuba ambayo alisifu "utulivu wa kijamii uliopatikana kwa bidii".

Katika jimbo la Xinjiang rais wa China Xi Jinping ametoa wito kwa viongozi wa jimbo hilo "kuhimiza zaidi kuchukia Uislamu na kudhibiti kikamilifu shughuli haramu za kidini".
Katika jimbo la Xinjiang rais wa China Xi Jinping ametoa wito kwa viongozi wa jimbo hilo "kuhimiza zaidi kuchukia Uislamu na kudhibiti kikamilifu shughuli haramu za kidini". © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu nchini China, Stéphane Lagarde

Rais wa China Xi Jinping anaendelea kusema: kipaumbele bado ni utulivu katika magharibi kuu ya China na hivyo kudumisha sera kali dhidi ya Waislamu walio wachache ambayo imelaaniwa kwa kiasi katika ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka uliyopita.

Ukaguzi na uhamisho

Kwa mujibu wa sehemu ya hotuba iliyochapishwa na Televisheni kuu ya China, rais wa China kwa mara nyingine aliangazia "mapambano dhidi ya ugaidi na kupinga kujitenga", mapambano dhidi ya "shughuli haramu za kidini" na "kuheshimu sheria" katika eneo linalojitawala la Uyghur ambalo bado linakumbukumbu za ghasia za mwaka 2009 na ukandamizaji uliofuatia. Kwa hakika, hii ina maana kwamba kuchafuliwa kwa Uislamu na uhamisho wa watu utaendelea.

Lugha ya Uyghur, ambayo zamani ilifundishwa katika shule katika eneo linalojitawala, imebadilishwa na mafundisho ya Mandarin. Na vijana kutoka jamii ya Waislamu walio wachache hutumwa mara kwa mara kwenye viwanda vya pwani ya mashariki ya China kwa jina la maendeleo ya kiuchumi, nguzo ya "utulivu wa kijamii". Matokeo: Hans - kabila kubwa zaidi nchini China - sasa wanawakilisha 41% ya wakazi wa Xinjiang dhidi ya 200,000 wakati Jamhuri ya Watu wa China ilipoundwa mnamo mwaka 1949, shirika la habari la AFP linakumbusha.

Kurudi kutoka mkutano wa kilele wa BRICS 

Hii ni mara ya pili kwa rais wa China kutembelea eneo la China magharibi katika kipindi cha miaka tisa. Ziara ya mwisho ilifanyika msimu wa joto mwaka uliyopita. Xi Jinping kisha akatangaza kwamba Xinjiang ni "kitovu kikuu cha kuunganisha China na nchi nyingine", huku akikaribisha "matokeo yenye matunda" ya Mpango wa Belt and Road - barabara mpya za hariri za China ambazo zimeiwezesha China kuharakisha biashara na uwekezaji wake katika miundombinu, hasa na Asia na Afrika.

Ziara hii pia ni hatua ya kushtukiza katika kurudi kutoka kwa mkutano wa kilele wa BRICS huko Pretoria, ambapo China ilitetea upanuzi wa muungao huo. Kwa hiyo pia ni sehemu ya mazungumzo mapana, hasa na viongozi wa nchi za "Global South" waliokutana Afrika Kusini. Huko Urumqi, mji mkuu wa jimbo linalojitawala la Uyghur, Xi Jinping hivyo alitetea matumizi ya propaganda chanya inayoonyesha Xinjiang "nzuri na yenye tabasamu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.