Pata taarifa kuu

Rais Xi kuzuru Afrika Kusini wiki ijayo

Mamlaka nchini Afrika Kusini zimethibitisha kwamba rais wa China Xi Jinping anatarajiwa kufanya ziara nchini humo wiki ijayo ambapo pia atahudhuria mkutano wa Brics.

Rais Xi anatarajiwa kuzuru Afrika Kusini wiki ijayo
Rais Xi anatarajiwa kuzuru Afrika Kusini wiki ijayo AP - Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Brics ni muungano wa nchi za Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini , muungano ambayo baadhi wameuona kama mbadala wa kundi la G7 la mataifa yalioimarika.

Hii ni ziara ya pili ya kimataifa ya rais Xi mwaka huu, baada ya ile aliyoifanya nchini Urusi mwezi Machi.

Ziara hii pia inakuja wakati huu viongozi wa Brics wakitarajiwa kukutana wiki ijayo, mpango wa kuendeleza unachama wa muungano huo ukiwa sehemu ya agenda ya kikao hicho.

Tayari baadhi ya mataifa ya Afrika ikiwemo Algeria, Misiri na Ethiopia, yameonyesha nia ya kupata uanachama wa muungano huo.

Maswali yalikuwa yameibuka iwapo rais wa Urusi angehudhuria kikao hicho, japokuwa afisi ya rais wa Afrika Kusini ilithibitisha kwamba hatahudhuria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.