Pata taarifa kuu

India: Idadi ya waliofariki kutokana na maporomoko ya udongo yafikia 27

Idadi ya vifo kutokana na maporomoko makubwa ya ardhi katika jimbo la Maharashtra magharibi mwa India imeongezeka hadi 27 siku ya Jumapili na takriban watu 50 bado hawajulikani walipo, mamlaka imesema. Siku ya Alhamisi, mvua kuwa zilisababisha maporomoko ya ardhi katika kijiji kimoja wilaya ya Raigad, eneo lenye milima na misitu takriban kilomita 100 kutoka Mumbai.

Picha iliyotolewa na Kikosi cha Kitaifa cha Kukabiliana na Maafa nchini India (NDRF) ikionyesha wafanyakazi wa NDRF wakijaribu kuwaokoa raia waliokwama kwenye mto Beas uliofurika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha karibu na kijiji cha Nagwayin, wilaya ya Mandi, Himachal Pradesh Jumapili, Julai 9, 2023.
Picha iliyotolewa na Kikosi cha Kitaifa cha Kukabiliana na Maafa nchini India (NDRF) ikionyesha wafanyakazi wa NDRF wakijaribu kuwaokoa raia waliokwama kwenye mto Beas uliofurika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha karibu na kijiji cha Nagwayin, wilaya ya Mandi, Himachal Pradesh Jumapili, Julai 9, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

"Tumehesabu maiti 27 kufikia sasa, na kati ya watu 50 na 60 bado hawajulikani walipo, lakini kuna matatizo mengi katika kazi ya uokoaji katika eneo hilo," ofisa wa eneo hilo Yogesh Mhase ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili.

Ripoti ya awali ilitaja takriban watu kumi na sita waliofariki.

Yogesh Mhase amesema kitongoji hicho kilikuwa takriban kilomita tano kutoka barabara ya karibu.

Familia kadhaa zilizoangamia

"Hakuna vifaa vizito vinavyoweza kufika kwenye eneo hili, tuna mashine ndogo tu na kazi nyingi zinapaswa kufanywa kwa mikono," ameongeza Yogesh Mhase.

"Mvua kubwa ambazo hazijakoma katika eneo hili pia zinafanya operesheni kuwa ngumu zaidi," amebainisha, akisema hana matumaini juu ya uwezekano wa kupata manusura wengine katika siku ya nne ya operesheni inayoendelea ya uokoaji.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, familia kadhaa ziliuawa.

Tangu kuanza kwa mvua nchini India mapema mwezi Juni, mafuriko na maporomoko ya ardhi yamesababisha vifo vya makumi ya watu nchini humo. Wataalamu wanaamini kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaongeza idadi ya matukio ya hali mbaya ya hewa duniani kote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.