Pata taarifa kuu
ULINZI-DIPLOMASIA

Julai 14: Emmanuel Macron na Narendra Modi wahudhuria gwaride la kijeshi

Gwaride la Julai 14 limefanyika Ijumaa hii asubuhi kwenye Champs-Élysées huko Paris. Mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, amehudhuria na mwenyeji wake, rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, baada ya kupokea tuzo la Heshima kutokakitengo cha jeshi, tuzo ya juu zaidi nchini Ufaransa.

Emmanuel Macron na Narendra Modi, wakati wa gwaride la Julai 14, kwenye mtaa wa Champs-Élysées, mjini Paris.
Emmanuel Macron na Narendra Modi, wakati wa gwaride la Julai 14, kwenye mtaa wa Champs-Élysées, mjini Paris. AFP - GONZALO FUENTES
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya washiriki 6,000 na vyombo zaidi ya mia moja vya anga vilionekana kwenye barabara ya avenue des Champs-Élysées, mjini Paris, kwa gwaride la jadi la Julai 14. viongozi wa heshima waliohudhuria gwaride hilo ni, rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, mgeni wa heshima mwaka huu.

Katika utangulizi wa gwaride hilo, mkuu wa nchi wa Ufaransa alishuka katika gari la kijeshi kwenye barabara ya kifahari ya Paris mbele ya umati wa watu, akilakiwa kwa makofi, lakini pia shangwe na vigelegele.

Baada ya burudani ya muziki ambayo ilishiriki nchi kumi na mbili zilizoisaidia Ufaransa wakati wa muongo wa ushiriki wa kijeshi huko Sahel, ndege tisa za Ulinzi-doria za Ufaransa ziliruka juu ya anga ya Paris na kuipaka rangi ya bluu, nyeupe, nyekundu, ikifuatiwa na ndege tatu za India.

Askari wa Kihindi wakiwa na vilemba

Gwaride la askari kwa miguu lilianza muda mfupi kabla ya tano mchana. Katika ufunguzi huo, wanajeshi 240 kutoka vikosi vya India, baadhi wakiwa wamevalia vilemba, walishiriki gwaride hili hadi eneo la Place de la Concorde. Ufaransa na India zinasherehekea kumbukumbu ya miaka 25 ya ushirikiano wao wa kimkakati mwaka huu, ambao Paris inalenga kuimarisha ili kupima uzito katika ukanda wa Asia-Pacific, ingawa India inashutumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kutumia hatua za kimabavu.

Wanajeshi wa India wakati wa gwaride la Julai 14 kwenye mtaa wa Champs-Élysées mjini Paris, Julai 14, 2023.
Wanajeshi wa India wakati wa gwaride la Julai 14 kwenye mtaa wa Champs-Élysées mjini Paris, Julai 14, 2023. AP - Christophe Ena
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.