Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini yarusha 'makombora kadhaa ya cruise ' kwenye Bahari ya Manjano

Mvutano umekuwa ukiongezeka kati ya Korea mbili tangu Jumanne. Jumamosi hii, Pyongyang imerusha makombora mapya kuelekea baharini.

Wakaazi wanatazama habari za kurushwa kwa makombora ya Korea Kaskazini mnamo Julai 22, 2023, huko Seoul.
Wakaazi wanatazama habari za kurushwa kwa makombora ya Korea Kaskazini mnamo Julai 22, 2023, huko Seoul. AFP - JUNG YEON-JE
Matangazo ya kibiashara

Urushaji wa makombora ya Korea Kaskazini umefanyika mwendo wa saa nne asubuhi kwa saa za huko, kulingana na makao maku ya majeshi huko Seoul. Tukio hili linakuja siku tatu baada ya urushaji wa makombora mawili ya Balestiki, katika Bahari ya Japani, kwenye pwani ya mashariki iliyo kinyume. "Ujasusi wa Korea Kusini na Marekani wanatathmini uzinduzi huu wa kurusha makombora, huku wakifuatilia dalili za shughuli za ziada," jeshi la Korea Kusini limeongeza.

Jaribio hili jipya la kijeshi pia linakuja siku mbili baada ya manowari ya nyuklia ya Marekani USS Kentucky kusimama Jumanne katika bandari ya Busan nchini Korea Kusini. kwa mara ya kwanza katika miaka arobaini, anaripoti mwandishi wetu huko Seoul, Célio Fioretti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.