Pata taarifa kuu

Japani: Rekodi ya wimbi la joto yawalazimu wakazi wa Tokyo kupunguza shughuli zao

Japan inaandamwa na viwango vya joto vilivyorekodiwa kwa zaidi ya wiki moja, pamoja na mvua kali kaskazini mwa nchi hiyo. Zebaki imefikia nyuzijoto 39.7°C Jumanne hii katika baadhi ya maeneo. Serikali imetoa tahadhari kuhusu hali ya joto kali kwa wilaya 20 kati ya 47 za nchi hiyo. Makumi ya mamilioni ya watu wanahusika na arifa hizi.

Umati wa watu wakitumia miavuli kutokaa na kali huko Tokyo mnamo Julai 17, 2023.
Umati wa watu wakitumia miavuli kutokaa na kali huko Tokyo mnamo Julai 17, 2023. AP - Kiichiro Sato
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Tokyo, Frédéric Charles

Tokyo inakabiliwa na siku yake ya sita mfululizo kwa zaidi ya nyuzijoto 35°C na kiwango cha unyevu cha zaidi ya 70%. Ni mwaka wa pili mfululizo kwa Japani kupata joto la juu kama hilo mnamo mwezi Julai, tangu data kama hiyo irekodiwe mnamo 1875 karibu karne moja na nusu iliyopita.

Maelfu kadhaa ya watu wamelazwa hospitalini kutokana na kiharusi cha joto, ambacho kinaweza kuharibu ubongo au figo, kusababisha mashambulizi ya moyo na matatizo ya kupumua. Kila mwaka, wimbi la joto linaua katika nchi hii yenye watu wengi wanaozeeka kwa kasi, watu mia kadhaa.

Wito kuhifadhi umeme

Joto hili lenye unyevunyevu mwingi linatarajiwa kuendelea kwa wiki chache zijazo. Serikali inatoa wito kwa wakazi wa Tokyo kuhifadhi nishati ya umeme, hasa kati ya saa tisa alaasiri na saa kumi na mbili jioni. Huu ndio wakati wa siku ambapo hifadhi ya nishati iko chini kabisa. Inaweza kuwa chini ya 3% inayohitajika ili kuhakikisha usambazaji wa nishati thabiti. Alasiri, wakazi wa Tokyo wanaombwa kupunguza matumizi ya lifti, kuzima taa zisizo za lazima. Japan inajitahidi kuanzisha upya vinu vyake vya nguvu za nyuklia, ambavyo vimefungwa tangu ajali ya Fukushima mnamo Machi 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.