Pata taarifa kuu

Japani yaruhusiwa kutiririsha maji ya kinu cha nyuklia cha Fukushima baharini

Japan imepewa idhni kutoka kwa shirika la Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ili kumwaga katika Bahari ya Pasifiki sehemu ya maji yaliyosafishwa kutoka kwa kinu cha nyuklia cha Fukushima kilichoharibiwa, Machi 11, 2011, na tetemeko la ardhi na Tsunami kubwa. Na hii, licha ya upinzani wa jumuiya ya wavuvi ya Fukushima na China.

Japan imepewa idhni kutoka kwa shirika la Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ili kumwaga katika Bahari ya Pasifiki sehemu ya maji yaliyosafishwa kutoka kwa kinu cha nyuklia cha Fukushima kilichoharibiwa, Machi 11, 2011, na tetemeko la ardhi na tsunami kubwa.
Japan imepewa idhni kutoka kwa shirika la Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ili kumwaga katika Bahari ya Pasifiki sehemu ya maji yaliyosafishwa kutoka kwa kinu cha nyuklia cha Fukushima kilichoharibiwa, Machi 11, 2011, na tetemeko la ardhi na tsunami kubwa. AP - Hiro Komae
Matangazo ya kibiashara

Akiwa ziarani Tokyo, mkuu wa IAEA, Rafael Grossi, alimweleza Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida kuhusu matokeo ya uchambuzi wa usalama wa miaka miwili uliofanywa na shirika hilo la Umoja wa Mataifa. IAEA inahitimisha kuwa mpango wa Japan wa kutiririsha maji kutoka kwa mtambo wa Fukushima baharini unaafiki viwango vya kimataifa.

Mkurugenzi mkuu wa IAEA, Rafael Grossi, anatangaza kwamba athari za radiolojia kwa raia na mazingira ya maji yaliyosindikwa upya ya kituo cha nyuklia cha Fukushima ambayo yatamwagwa baharini hazitazingatiwa, anaripoti mwandishi wetu huko Tokyo, Frédéric Charles. Maki haya yatatiririshwa hatua kwa hatua. TEPCO, kampuni inayosimamia mtambo wa Fukushima, itafutilia mbali katika miaka thelathini kiwango cha tritium ambacho kituo cha nyuklia cha Hague nchini Ufaransa kinatiririsha ndani ya siku thelathini. 

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.