Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

China: Wanne wakamatwa baada ya mlipuko ulioua 31 katika mkahawa

Polisi nchini China imewakamata watu wanne kuhusiana na mlipuko ulioua takriban watu 31 jioni ya Jumatano (Juni 21) katika mgahawa mmoja kaskazini magharibi mwa China, Shirika la Habari la serikali la Xinhua limeripoti leo Jumamosi.

Maafisa wa kikosi cha Zima moto nchini China wakijaribu kudhibiti moto ulioua takriban watu 31 kwenye mgahawa katika mji wa Yinchuan mnamo Juni 21, 2023.
Maafisa wa kikosi cha Zima moto nchini China wakijaribu kudhibiti moto ulioua takriban watu 31 kwenye mgahawa katika mji wa Yinchuan mnamo Juni 21, 2023. AP - Wang Peng
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ambao pia ulijeruhi watu saba, ulisababishwa na uvujaji wa gesi ya petroli iliyoyeyuka, kwa mujibu wa mamlaka ya China.

Mlipuko huo ulitokea katika eneo la makazi la mji wa Yinchuan katika mkesha wa tamasha la Dragon Boat, sherehe ya siku tatu ambayo watu wengi wa China hukusanyika pamoja na familia na marafiki.

Washukiwa wanne waliokamatwa - mmiliki wa mgahawa, meneja na wanahisa wawili - wanatuhumiwa "kusababisha ajali mbaya kwa uzembe", na uchunguzi wa uhalifu unaendelea, shirika la habari la serikali la Xinhua limesema.

Mamlaka pia imezuia mali zao, pamoja na zile za watu wengine watano, shirika hili la habari limeongeza.

Baada ya mlipuko huo, Rais Xi Jinping wa China alitaka hasa juhudi zote zihamasishwe kwa ajili ya "kuimarisha uratibu na usimamizi wa usalama katika makampuni na maeneo muhimu ili kulinda raia na mali kwa ufanisi," kulingana na shirika la habari la New China.

Ajali za mara kwa mara

Milipuko hii na matukio mengine mabaya hutokea mara kwa mara nchini China, ambapo viwango vya sekta ya ujenzi mara nyingi havifikiwi. Kwa kuongeza, ujenzi usioidhinishwa ni mwingi nchini China na unaweza, kwa mfano katika kesi ya moto, kufanya iwe vigumu kwa watu ndani ya jengo kuepuka mkasa wa moto.

Mwezi Septemba mwaka uliyopita, takriban watu 17 walifariki kufuati mkasa wa moto katika mgahawa huko Changchun (kaskazini mashariki), kulingana na ripoti iliyotolewa na mamlaka.

Mnamo mwezi Januari 2022, mlipuko uliosababishwa na kinachoshukiwa kuwa gesi katika kantini uligharimu maisha ya zaidi ya watu kumi na wawili huko Chongqing (kusini-magharibi).

Mnamo mwezi Juni 2021, mlipuko wa gesi ambao uliharibu makazi ya watu huko Shiyan (katikati) uliua watu 25.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.