Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Thelathini na moja wauawa na mlipuko katika mgahawa mmoja nchini China

Takriban watu 31 wameuawa hivi punde katika mlipuko uliotokea kwenye mgahawa katika mji wa Yinchuan kaskazini magharibi mwa China Jumatano usiku, Shirika rasmi la Habari la Xinhua limeripoti leo Alhamisi.

Maafisa wa kikosi cha Zima moto huko Beijing mnamo Desemba 26, 2018.
Maafisa wa kikosi cha Zima moto huko Beijing mnamo Desemba 26, 2018. © Nicolas Asfouri
Matangazo ya kibiashara

"Kuvuja kwa gesi ya petroli iliyoyeyuka (...) kumesababisha mlipuko wakati wa huduma ya mgahawa wa nyama choma," shirika hilo limesema, likinukuu kamati ya kikanda ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP).

Watu wengine saba wanapokea matibabu, mmoja wao akiwa katika "hali mbaya", Xinhua imesema.

Waathiriwa wengine wawili waliungua vibaya sana, wengine wawili wamepata majeraha madogo, na wengine wawili wamepigwa na vipande vya vioo, kulingana na chanzo kimoja.

Kanda za video kutoka kwa televisheni ya serikali ya CCTV zimeonyesha zaidi ya maafisa kumi wa kikosi cha Zima moto wakipambana na moshi unaofuka kupitia shimo lililotokana na mlipuko huo. Mtaa huo unaofanyia biashara nyingine za vyakula na burudani ulikuwa umetapakaa vifusi.

Mlipuko huo ulitokea mwendo wa mbili na dakika arobani usiku saa za China (sawa na saa tano na dakika arobani saa za Afrika ya Mashariki) katika Mkahawa wa Fuyang Barbecue, ulioko katika eneo la makazi katikati mwa jiji la Yinchuan, mji mkuu wa Mkoa unaojitawala wa Ningxia.

Mkasa huo ulitokea siku moja kabla ya tamasha la Dragon Boat, sherehe ya siku tatu ambayo watu wengi wa China hukusanyika pamoja na familia na marafiki.

Rais Xi Jinping wa China ameomba juhudi zote zifanywe katika "kuwatunza waliojeruhiwa na kuimarisha usimamizi wa usalama katika makampuni na sekta muhimu ili kulinda maisha na mali za raia." ", imeripoti CCTV leo Alhamisi.

Wizara ya Usimamizi wa Dharura amesema kuwa kikosi cha Zima moto na uokoaji kimetuma zaidi ya maafisa 100 na magari 20 kwenye eneo la tukio baada ya mlipuko huo.

Shughuli za kutoa msaada zilimalizika saa kumi alfajiri siku ya Alhamisi saa za China (sawa na saa saba usiku saa za Afrika Mashariki), wizara imeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.