Pata taarifa kuu

China: Ndege yaanguka ikiwa na watu 133

Ndege ya shirika la ndege la China Eastern Airlines imeanguka kusini magharibi mwa nchi hiyo, kulingana na vyombo vya habari vya China. Idara ya huduma za dharura inaendelea kutafuta waathiriwa.

Ndege ya shirika la ndege la China Eastern Airlines iliyokuwa na abiria 133 imeanguka Machi 21, 2022 katika milima ya kusini mwa China.
Ndege ya shirika la ndege la China Eastern Airlines iliyokuwa na abiria 133 imeanguka Machi 21, 2022 katika milima ya kusini mwa China. AP - Ng Han Guan
Matangazo ya kibiashara

Sababu za ajali hiyo bado hazijajulikana. Ndege ya shirika la ndege la China Eastern Airlines iliyokuwa na watu 133 ilianguka kusini magharibi mwa China siku ya Jumatatu, televisheni ya taifa imeripoti, bila kutoa maelezo zaidi. Ndege hiyo aina ya Boeing-737, imeanguka karibu na mji wa Wuzhou, katika eneo la Guangxi, na "kusababisha moto kuzuka kwenye mlima", kimesema kituo cha CCTV, na kuongeza kuwa timu za waokoaji zilitumwa kwenye eneo la tukio.

"Tukio hili lilitokea Jumatatu kwa ndege ya abiria ya shirika la ndege la China Eastern Airlines ikiwa na watu 133 huko Guangxi, nchini China. Kazi ya uokoaji inaendelea. Idadi ya waliofariki haijulikani,” kulingana na vyombo vya habari vya serikali People’s Daily.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, safari ya ndege ya shirika la ndege la China Eastern Airlines yenye chapaa MU5735 illiruka muda mfupi baada ya saa moja jioni saa za China kutoka jiji kuu la kusini-magharibi la Kunming. Ilikuwa inaelekea katika mji wa Canton, kilomita 1,300 na uanja wa ndege ilikotoka. Ajali kubwa ya mwisho ya ndege nchini China ilitokeamwezi wa Agosti 2010 na iliua watu 42.

Taarifa zaidi zinakuja

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.