Pata taarifa kuu

Lula azuru China ili kufufua uhusiano kati ya China na Brazil

Lula anaanza, Jumanne hii, Aprili 11, 2023, ziara rasmi nchini China, hadi Aprili 14. Ziara hiyo ilipangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Machi, lakini rais wa Brazil alilazimika kuahirisha safari yake kwa sababu ya nimonia.

Rais wa Brazil Lula na mkewe Rosangela Silva mjini Brasilia Aprili 4, 2023.
Rais wa Brazil Lula na mkewe Rosangela Silva mjini Brasilia Aprili 4, 2023. AP - Eraldo Peres
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa mrengo mkali wa kulia Jair Bolsonaro (2019-2022) amerudi kusema kwamba China "inainunua Brazil" na alizidisha kauli kama hizi dhidi ya China, hasa wakati wa kampeni yake ya uchaguzi. Lula, aliyerejea madarakani tangu Januari 1, kwa hiyo anatafuta kuachana na hotuba hizi za uhasama na kuvunja kutengwa kidiplomasia kwa nchi yake, ili kuiweka Brazil kama kiungo muhimu duniani.

"Brazili inaendelea kuomba nafasi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ingawa  haina bahati ya kuipata", amesema mwanajiografia Hervé Théry, profesa katika Chuo Kikuu cha Sao Paolo. "Ni sehemu ya jaribio la kujiimarisha kidogo kati ya nchi hizi: Brazil wakati mwingine inajaribu kujiunga na klabu ya wababe, kwa mfano kwa kuwania katika OECD, na wakati mwingine kujifanya kama kiongozi wa kile wanachokiita Ulimwengu wa Tatu. "Brazil pia inajaribu kufufua Brics, klabu hii ya nchi zinazoendelea, ambayo inaleta pamoja Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini.

Upatanishi nchini Ukraine

Katika mkakati huu wa kidiplomasia, Lula pia anajaribu kujiweka kama mpatanishi katika vita vya Ukraine. Chini ya mihula yake miwili ya kwanza, kati ya 2003 na 2010, Brasilia ilikuwa tayari imejaribu kuwa msuluhishi katika faili ya nyuklia ya Irani. Leo, nchi hii ina msimamo usio na utata juu ya vita vya Ukraine. Kwa upande mmoja, Lula anasema Urusi haiwezi kunyakua ardhi kutoka Ukraine, lakini kwa upande mwingine, rais wa Brazil alipendekeza wiki iliyopita kwamba Ukraine inaweza kukabidhi Crimea kwa Urusi. Aidha, Brazil haishiriki katika vikwazo dhidi ya Moscow.

Katika ziara yake nchini China, Lula anakusudia kuwasilisha mpango wake wa upatanishi wa amani nchini Ukraine kwa mwenzake Xi Jinping. Kwa Frédéric Louault (*), profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu Huria cha Brussels (ULB), hii ni sehemu ya utamaduni wa zamani wa kidiplomasia nchini Brazili. "Lula, wakati wa utawala wake wa kwanza, alianzisha uhusiano mzuri na Urusi, bila kuitenga kabisa Marekani, Umoja wa Ulaya na kambi ya Magharibi," anaelezea.

"Brazil ina nafasi ya mpatanishi ambayo inaweza kuleta pamoja kwenye meza moja ya mazunguzo wadau tofauti ambao wanapingana vikali", anaendelea mtafiti. Hii ndiyo sababu pia Brazili inahitaji kupendekeza suluhisho lililofafanuliwa na mataifa mengine yenye nguvu, hasa China. Iwapo itafanya kazi, na kwamba "msimamo wa kawaida wa China na Brazili unaweza kufanya iwezekane kuwaweka wahusika mbalimbali katika mzozo kwenye meza moja ya mazungumzo", Brasilia inaweza kutoka nayo vyema katika anga ya kimataifa, amebaini Frédéric Louault.

China ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Brazil, hivyo uchumi ni sehemu muhimu ya ziara ya Lula nchini China. Soko la China linawakilisha zaidi ya theluthi ya mauzo ya nje ya Brazil, mara tatu zaidi ya Marekani. Brazili ni mojawapo ya nchi chache zinazouza zaidi China kuliko inavyonunua kutoka kwayo, hususan maharagwe,  soya au nyama ya ng'ombe ya Brazili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.