Pata taarifa kuu

Rais wa Brazil Lula da Silva kuzuru China

NAIROBI – Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva atazuru China mwishoni mwa mwezi huu mwa Machi, wizara ya mambo ya nje ya Beijing imethibitisha Ijumaa.

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva REUTERS - ADRIANO MACHADO
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa mambo ya nje wa ChinaHua Chunying, Lula, anatarajiwa jijini Beijing kwa mwaliko wa rais wa China Xi Jinping kati ya tarehe 26 hadi 31.

Kiongozi huyo, ailyewahi kuwa rais wa Brazil kati ya mwaka wa 2003 na 2010 kabla ya kurejea tena madarakani mwanzoni mwa mwaka huu ,ameonyesha nia ya kurejesha nchi yake katika jukwa la kiamatifa baada ya kuonekana kutengwa na utawala wa mtangulizi wake Jair Bolsonaro.

Lula ameelezea haja ya kuanzisha  tena uhusiano mzuri na China tofauti kabisa na Bolsonaro, ziara hii ikiwa ya kwanza kwa Lula nchini China tangu aingie madarakani mwezi Januari mwaka huu, China ikiwa ni mshirika mkubwa  wa kibiashara wa Brazili.

Ziara ya Luiz Inacio Lula da Silva nchini China imetangazwa wakati ambapo rais wa China Xi Jinping akitarajiwa kufanya ziara ya kiserikali nchini  Urusi wiki ijayo, wizara ya mambo ya nje ya Beijing imethibitisha siku ya Ijumaa, ikiwa ni safari yake ya kwanza mjini Moscow katika takriban kipindi cha miaka minne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.