Pata taarifa kuu

Takriban watu wanne wafariki katika mlipuko wa bomu kusini magharibi mwa Pakistan

Takriban watu wanne wameuawa na 15 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliolenga gari la polisi kusini magharibi mwa Pakistan Jumatatu, polisi ya eneo hilo imesema. 

Askari wa jeshi la Pakistan akiwa amesimama juu ya paa ya moja yamajengo ya makao makuu ya polisi, siku moja baada ya shambulio la Taliban, huko Karachi Jumamosi hii Februari 18, 2023.
Askari wa jeshi la Pakistan akiwa amesimama juu ya paa ya moja yamajengo ya makao makuu ya polisi, siku moja baada ya shambulio la Taliban, huko Karachi Jumamosi hii Februari 18, 2023. AP - Ikram Suri
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulitokea katika soko lenye shughuli nyingi huko Quetta, mji mkuu wa jimbo la Balochistan, ambapo makundi ya wakaazi wanaotaka kujitenga na wapiganaji wa Kiislamu wenye silaha mara kwa mara hufanya mashambulizi yanayolenga jeshi au polisi.

Takriban watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa siku ya Jumatatu katika mlipuko uliolenga gari la polisi katika mkoa wa kusini magharibi wa Balochistan nchini Pakistan, polisi na vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Takriban majeruhi 15, wakiwemo maafisa wa polisi, wamesafirishwa hadi hospitali ya eneo hilo.

Magari kadhaa, zikiwemo pikipiki, yaliyokuwa yameegeshwa kando ya barabara pia yaliharibiwa na mlipuko huo.

Kanda za video zilizotolewa na kituo cha ndani cha Dawn News zinaonyesha sehemu ya barabara ikiwa imejaa vioo vilivyovunjika, vipande vya vitambaa, viatu na vipande vya chuma vya magari yaliyoharibika.

Hakuna upande wowote uliodai kuhusika na mlipuko huo, ingawa makundi yanayojitenga ya Baloch na wafuasi wa kundi mama la Taliban la Pakistani, Tehreek-e-Taliban Pakistan, kwa muda mrefu wameshambulia vikosi vya usalama katika jimbo hili lenye utajiri wa madini.

Balochistan ni jimbo kubwa zaidi la Pakistan, lakini pia jimbo maskini zaidi. Vikosi vya usalama vimekuwa vikikabiliana kwa muda mrefu na watu wanaotaka kujitenga kwa Baloch, ambao wanajihusisha na vitendo vya uasi.

Jimbo hilo pia ni mhimili mkuu wa Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan wenye thamani ya dola bilioni 64, unaolenga kuunganisha mkoa wa kimkakati wa Xinjiang kaskazini magharibi mwa China na bandari ya Gawadar huko Balochistan, kutokana na mtandao wa barabara na reli kwa usafirishaji wa bidhaa , lakini pia mabomba ya mafuta na gesi kwa ajili ya usafirishaji wa mafuta na gesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.