Pata taarifa kuu
PAKISTANI- USALAMA -AFYA-UCHUMI

UN yaomba jumuiya ya kimataifa kuisaidia Pakistani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress, ameomba jumuiya ya Kimataifa, kuisaidia Pakistan, kujenga upya miundo yake, baada ya mafuriko ya mwaka uliopita, yaliyosababisha uharibifu mkubwa.

Antonio Guterres katibu Mkuu wa UN
Antonio Guterres katibu Mkuu wa UN AP - Thomas Hartwell
Matangazo ya kibiashara

Guteress amesema Dola Bilioni 16.3 zinahitajika ili kuijenga miundo mbinu kama barabara na maakazi ya watu baada ya watu zaidia ya 1700 kupoteza maisha na wengine kuathiriwa.

“Lazima jibu letu kwa raia wa Pakistan, liendane na juhudi zetu za uwekezaji mkubwa wa kuimarisha jamii nchini humo katika siku zijazo.” amesema Antonio Guteress

Baadhi ya mataifa mengine ya dunia nayo pia yameonekana kukabiliwa na tatizo la mafuriko yanayochangiwa pakubwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.