Pata taarifa kuu

Pakistani: Mlipuko katika msikiti huko Peshawar waua watu wengi

Takriban watu 25 wameuawa na wengine 120 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea leo Jumatatu kwenye msikiti mmoja ndani ya makao makuu ya polisi huko Peshawar, kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Pakistani: mlipuko katika msikiti mmoja huko Peshawar, kaskazini-magharibi mwa nchi Jumatatu hii, Januari 30, umeua watu wasiopungua ishirini na wengine wengi kujeruhiwa.
Pakistani: mlipuko katika msikiti mmoja huko Peshawar, kaskazini-magharibi mwa nchi Jumatatu hii, Januari 30, umeua watu wasiopungua ishirini na wengine wengi kujeruhiwa. AFP - MAAZ ALI
Matangazo ya kibiashara

"Kwa sasa, kipaumbele chetu kikuu ni kuokoa watu walionaswa chini ya vifusi," Shaffiullah Khan, afisa mkuu wa utawala katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, ambalo Peshawar ndio mji mkuu wake, ameliambia shirika la habari la AFP.

Mlipuko huo ulikuwa wa nguvu, anasema mkazi wa Peshawar, akihojiwa na mwanahabari wetu, Sonia Ghezali. Mlipuko huo ulitokea karibu saba: na dakika arobani, wakati wa sala ya alasiri. Waumini wengi walikuwa katika ibada wakati mlipuko huo ulipotokea.

Kulingana na baadhi ya vyanzo vya usalama, mshambuliaji wa kujitoa mhanga, ambaye alikuwa safa ya mbele msikitini, alilipua mkanada wake uliojaa vilipuzi wakati sala ikiendelea. Uchunguzi umefunguliwa ili kuthibitisha maelezo haya ya awali.

Hakuna kundi ambalo limedai shambulizi hili, lakini kundi la TTP (Tehreek-e-Taliban Pakistan) linanyooshewa kidole.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.