Pata taarifa kuu

Korea Kusini: Kiongozi wa zamani Lee Myung-bak aachiliwa huru kwa msamaha wa rais

Hatimaye rais wa zamani wa Korea Kusini aliyehukumiwa kifungo, ameachiliwa huru kwa msamaha wa rais. Baada ya Park Geun-hye kupewa msamaha wa rais mnamo mwaka 2021, ni zamu ya rais wa zamani, Lee Myung-bak, kupokea msamaha wa rais. Kiongozi huyu wa zamani alihukumiwa kifungo cha miaka 17 jela kwa ufisadi na ubadhirifu.

Rais wa zamani wa Korea Kusini Lee Myung-bak, katikati, wakati wa kesi yake ya kwanza Mei 23, 2018 huko Seoul.
Rais wa zamani wa Korea Kusini Lee Myung-bak, katikati, wakati wa kesi yake ya kwanza Mei 23, 2018 huko Seoul. © Chung Sung-Jun / AP
Matangazo ya kibiashara

Hata kama uamuzi unaowezekana katika mwelekeo huu ulitangazwa kwenye vyombo vya habari katika siku za hivi karibuni, bado ni ishara kali ya kisiasa kutoka kwa rais wa kihafidhina Yoon Suk-yeol.

Ni miaka kumi na mitano jela, na karibu dola milioni 16 za faini ambazo zinatoweka kwa uamuzi wa rais, kuanzia siku ya Jumatano, Desemba 28. Lee Myung-bak, rais wa Korea Kusini kuanzia mwaka 2008 hadi 2013 na sasa ana umri wa miaka 81, anasema msamaha huu wa kirais unamuondoa sehemu mbaya, kwani pamoja na kufutwa kwa kifungo chake, atapata marupurupu yake ifikapo siku Jumatano.

Lee Myung-bak alihukumiwa mwaka wa 2020 kwa ufisadi na ubadhirifu, kwa sababu alipatikana na hatia ya kupokea makumi ya mamilioni ya dola kama hongo, hasa kwa kubadilisha uamuuzi kwa msamaha kwa mkuu wa zamani wa Samsung. Lee Myung-bak aalifutiwa adhabu kwa sababu za kiafya na alikaa gerezani kwa miaka miwili pekee. Sasa ananufaika kwa muktadha wa kisiasa.

Mwishoni mwa uchaguzi wa mwezi Agosti, Rais wa sasa Yoon Suk-yeol hapo awali hakutaka kumsamehe mtu kama huyo mwenye utata. Kadiri kiwango chake cha umaarufu kinapoongezeka, anazidi kuchukua mstari wake wa kihafidhina. Baada ya kuwa na msimamo katika kukabiliana na mgomo wa madereva wa malori na kujizatiti vilivyo kwa faili ya Korea Kaskazini, Yoon anamsamehe mmoja wa watangulizi wake, moja ya alama za mrengo ngumu wa kulia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.