Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini yarusha makombora 4 ya masafa mafupi kuelekea baharini

Korea Kaskazini imerusha makombora manne ya masafa mafupi kuelekea Bahari ya Njano, jeshi la Korea Kusini limesema Jumamosi, baada ya rekodi ya ufyatuaji wa makombora yaliyorushwa na Pyongyang wiki hii.

Pyongyang ilirusha takriban makombora 30 siku ya Jumatano na Alhamisi, likiwemo lililomalizi mbio zake karibu na eneo la maji ya eneo la kusini kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Vita vya Korea mwaka 1953. Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol alizungumzia kitendo cha jeshi la Korea Kaskazini kama 'kitendo cha uvamizi' dhidi ya nchi yake.
Pyongyang ilirusha takriban makombora 30 siku ya Jumatano na Alhamisi, likiwemo lililomalizi mbio zake karibu na eneo la maji ya eneo la kusini kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Vita vya Korea mwaka 1953. Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol alizungumzia kitendo cha jeshi la Korea Kaskazini kama 'kitendo cha uvamizi' dhidi ya nchi yake. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Korea Kusini limegundua uzinduzi huo "kutoka Donglim, jimbo la Pyongan Kaskazini, kuelekea bahari ya magharibi, kati ya saa 11:32 na 11:39  (kati ya 2:32 asubuhi na 2:39 GMT) leo" Jumamosii, makao makuu ya majeshi ya Korea Kusini imesema katika taarifa, ikitumia jina lingine la Bahari ya Njano.

Mvutano uliokithiri

Pia Jumamosi hii, afisa wa Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini amethibitisha kwamba ndege ya kivita ya Marekani aina ya B-1B itashiriki katika mazoezi ya anga yanayoendelea nchini Korea Kusini ambayo yanafanywa kwa pamoja na Seoul na Washington siku ya Jumamosi.

Pyongyang ilirusha takriban makombora 30 siku ya Jumatano na Alhamisi, likiwemo lililomalizi mbio zake karibu na eneo la maji ya eneo la kusini kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Vita vya Korea mwaka 1953. Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol alizungumzia kitendo cha jeshi la Korea Kaskazini kama 'kitendo cha uvamizi' dhidi ya nchi yake.

Korea Kaskazini siku zote inayachukuliwa mazoezi ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini kama mazoezi ya uvamizi wa ardhi yake au kupindua utawala wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.