Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini yarusha karibu makombora 20, Seoul yalaani 'uvamizi wa ardhi yake'

Korea Kaskazini imerusha takriban makombora 23 siku ya Jumatano, moja ya makombora hayo yakianguka karibu na eneo la maji ya Korea Kusini, na hivyo kuzua mvutano mkali na jirani yake wa kusini ambaye amejibu kwa kurusha makombora matatu kuelekea baharini.

Huko Seoul, wakaazi wanatazama ujumbe wa onyo kwenye runinga baada ya makombora ya Korea Kaskazini kurushwa mnamo Novemba 2, 2022.
Huko Seoul, wakaazi wanatazama ujumbe wa onyo kwenye runinga baada ya makombora ya Korea Kaskazini kurushwa mnamo Novemba 2, 2022. REUTERS - YONHAP NEWS AGENCY
Matangazo ya kibiashara

Wakati jeshi la Korea Kusini kwa sasa linashiriki katika mazoezi makubwa ya pamoja ya anga katika historia yake na mshirika wake Marekani, Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol siku ya Jumatano ametaja kile alichokiita "uchokozi" wa Pyongyang, akilaani "uvamizi wa nchi yake".

Yote yalianza saa 8:51 asubuh. kwa saa za Korea Kusini, wakati makombora matatu ya masafa mafupi ya Korea Kaskazini yaliporushwa na moja kuvuka "Northern Limit Line", ambayo inaunda mpaka wa baharini kati ya nchi hizo mbili. Ikiwa ni mara ya  kwanza tangu mgawanyiko wa rasi hiyo baada ya Vita vya Korea mnamo 1953.

Baada ya hayo, tahadhari ya nadra ya uvamizi wa anga imetolewa katika kisiwa cha Korea Kusini cha Ulleungdo, kilichoko karibu kilomita 120 mashariki mwa rasi ya Korea, ambapo wakazi wameagizwa kukimbilia mahandaki. Wakazi waliombwa "kuhama hadi kwenye makazi ya chini ya ardhi ya karibu," ameripoti mwandishi wetu wa Seoul, Nicolas Rocca.

Moja ya makombora hayo yalimaliza mwendo wake baharini kilomita 57 tu kutoka mji wa Sokcho, kaskazini-mashariki mwa Korea Kusini, jeshi la Korea Kusini limesema, likiita uvurumishaji huo wa makombora kwa " ni kitu ambacho hakijawahi kutokea na kisichoweza kuvumilika". 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo mkurugenzi mkuu wa oparesheni katika jeshi la Korea Kusini Kang Shin Chul amesema waligundua makombora matatu ya masafa mafupi ya korea Kaskazini.

Amesema makombora hayo yaliondondoka katika pwani ya rasi ya mashariki na kuapa kwamba jeshi la nchi yake litajibu vikali kile alichokiita uchokozi wa jirani yake Korea Kaskazini .

"Ufyatuaji wa makombora wa leo kwa mara ya kwanza Kombora la Korea Kaskazini limetua karibu na eneo letu la pwani, kusini mwa mpaka wa bahari"

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.