Pata taarifa kuu

Belarus: Putin-Lukashenko wakutana wakati Ukraine ikikabiliwa na mashambulizi ya makombora

Kyiv na mikoa kumi ya Ukraine inakabiliwa na upungufu mpya wa umeme, baada ya wimbi jipya la mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yaliyozinduliwa na Urusi dhidi ya miundombinu ya nishati.

Magari ya kijeshi ya Urusi wakati wa mazoezi ya kijeshi yaliyofanyika Belarus, Desemba 19, 2022.
Magari ya kijeshi ya Urusi wakati wa mazoezi ya kijeshi yaliyofanyika Belarus, Desemba 19, 2022. © AP / Russian Defense Ministry Press Service
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya yalitokea saa chache kabla ya ziara ya Vladimir Putin kwenda Minsk. Rais wa Urusi ana miadi na mwenzake wa Belarus Alexander Lukashenko. Na swali moja liko akilini mwa kila mtu: je, rais wa Urusi anakusudia kumlazimisha mwenzake kushiriki moja kwa moja katika vita dhidi ya Ukraine?

Uwezekano wa Belarus kushiriki katika mapigano nchini Ukraine ni hali inayotia wasiwasi mamlaka huko Kyiv. Kwa hali yoyote wanaamini kwamba mashambulizi mapya kwenye mji mkuu wa Ukraine yatazinduliwa kutoka kwenye ardhi ya Belarus, katika wiki chache au miezi michache ijayo.

Mazoezi ya kimbinu

Hali hiyo tayari imetokea, mnamo mwezi wa Februari 2022, lakini wanajeshi wa Belarus walikuwa hawajashiriki katika shambulio la mji mkuu wa Ukraine. Wasiwasi huu umeongezeka kufuatia tangazo la mazoezi ya kimbinu na jeshi la Urusi nchini Belarus. Alexander Lukashenko ammesema na kususitiza kwamba hana mpango wa kutuma wanajeshi nchini Ukraine, lakini taarifa kutoka kwa wizara yake ya ulinzi inabaini kwamba imekamilisha mfululizo wa ukaguzi wa vikosi vya jeshi, hali ambayo inaongeza mkanganyiko.

Sehemu ya kisaikolojia

Baada ya ziara nne za kiongozi wa Belarus huko Moscow, Sochi na Saint Petersburg, Vladimir Putin anaenda Minsk kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu na nusu. Kama watazamaji kadhaa wanavyoona, haitaji kusafiri ili kulazimisha mkono wa mwenzake, ambaye anategemea sana Moscow. Lakini ziara hii ina, kwa hali yoyote, sehemu ya kisaikolojia. Inaongeza shinikizo kwa Kyiv. Katika hotuba iliyorekodiwa, Volodymyr Zelensky anasema kwamba nchi yake ilikuwa ikijiandaa "kwa hali zote zinazowezekana za ulinzi": "Ulinzi wa mpaka wetu, kwa upande wa Urusi au Belarus, anasema rais wa Ukraine, ni kipaumbele chetu cha kudumu ".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.