Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE MAPIGANO

Urusi imerusha makombora 76 katika maeneo tofauti nchini Ukraine

Wanajeshi wa Urusi, wamerusha makombora 76 katika maeneo mbalimbali ya Ukraine, hivi leo, likiwemo jiji kuu Kyiv na miji kadhaa ya nchi hiyo.

Jengo lililoharibia baada ya mashambulio ya Urusi nchini Ukraine
Jengo lililoharibia baada ya mashambulio ya Urusi nchini Ukraine AP - Emilio Morenatti
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa Ukraine wanasema watu wawili wameuawa mjini Kharkiv na wingine mjini Kherson kufuatia mashambulio ya makombora ambayo yamekuwa yakiendelea kwa siku nzima.

Mbali na kushambuliwa kwa makaazi ya watu, maofisa nchini humo wamesema, miundo mbinu ya nishati imeshambuliwa pia katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo inashuhudia kipindi cha baridi.

Katika jiji la Kyiv, inaripotiwa kuwa makombora 14 yalirushwa, ikiwa ndio mengi zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa siku moja, tangu vita kuanza mwezi Februari mwaka huu.

Uongozi wa Ukraine, umewaambia raia wake, kuwa makini kwa sababu Urusi inapanga kuongeza mashambulio, kuelekea mwaka mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.