Pata taarifa kuu

Zelensky atoa wito kwa Ulaya kuunga mkono kuundwa kwa Mahakama maalum, kuichunguza Urusi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ameyataka mataifa ya Ulaya, kusaidia kuundwa kwa Mahakama maalum, kuchunguza visa vya uhalifu wa kivita, vinavyodaiwa kutekelezwa kwa raia wake na wanajeshi wa Urusi.

Zelensky ameliambia Bunge la Ulaya kupitia hotuba ya video kuwa ni muhimu kwa mataifa ya Ulaya kuunga mkono kuundwa kwa mahakama hiyo
Zelensky ameliambia Bunge la Ulaya kupitia hotuba ya video kuwa ni muhimu kwa mataifa ya Ulaya kuunga mkono kuundwa kwa mahakama hiyo AP - Christophe Gateau
Matangazo ya kibiashara

Zelensky ameliambia Bunge la Ulaya kupitia hotuba ya video kuwa ni muhimu kwa mataifa ya Ulaya kuunga mkono kuundwa kwa mahakama hiyo. Ameyasema hayo alipokuwa akipokea tuzo ya juu kabisa inayotolewa kila mwaka na Umoja wa Ulaya ya Sakharov kwa niaba ya watu jasiri wa Ukraine. 

Hata hivyo amesisitiza kuwa watavishinda vikosi vya Moscow vilivyovamia nchi yake na kutoa pigo kubwa kwa malengo ya Rais wa Urusi Vladmir Putin. 

Katika hatua nyingine, Ukraine inasema, imefanikiwa kuachiwa kwa raia wa Marekani na raia wake 64 kutoka nchini Urusi, katika mpango wa kubadilishana wafungwa. 

Wakati huo huo maafisa wa Ukraine wanasema, wameangusha ndege kadhaa zisizokuwa na rubani kutoka Urusi, baada ya mashambulio yaliyolenga jiji kuu Kyiv. 

Mashambulio yalisikika katikati ya jii kuu Kyiev leo asubuhi kabla ya ndege hizo 13  kuagushwa na maafisa wa Ukraine, huku ripoti zikieleza kuwa, zilitengenezwa nchini Iran. 

Gavana na Kiev Oleksiy Kuleba ameishtumu Urusi kwa kuendelea kuishambulia Ukraine lakini pia kulenga miundo mbinu ya nishati hasa katika kipindi hiki cha baridi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.