Pata taarifa kuu

Ukraine: Kyiv yakumbwa na mashambulizi mapya, mitambo ya umeme yalengwa

Ndege zisizo na rubani za Urusi zilizotengenezwa na Iran zimetekeleza mashambulizi mapya kwenye mji mkuu, wa Urkraine, Kyiv Jumatano hii asubuhi. Ndege zisizo na rubani zote zimeharibiwa, kulingana na jeshi la Ukraine.

Kyiv, Ukraine: jengo lililokumbwa na mashambulizi ya anga Jumatano hii, Desemba 14, 2022.
Kyiv, Ukraine: jengo lililokumbwa na mashambulizi ya anga Jumatano hii, Desemba 14, 2022. AP - Evgeniy Maloletka
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisifu ufanisi wa vikosi vyake vya kupambana na mashambulizi ya angani, akisema ndege zote 13 zisizo na rubani za Shahed zilizotengenezwa na Iran zimetunguliwa. "Magaidi walianza mashambulizi yao asubuhi wakitumia ndege zisizo na ruban, Β Shahed 13," Bw. Zelensky amesema akizungumzia ndege zisizo na rubani za kujitoa mhanga. "Kwa mujibu wa taarifa za awali, ndege zote 13 zilidunguliwa kwa makombora na mfumo wetu wa ulinzi wa anga," aeongeza. Milipuko iliyosikika mapema Jumatano hii ni ile iliyosababishwa na uharibifu wa ndege hizi zisizo na rubani, anaripoti mwandishi wetu katika mji wa Kyiv, StΓ©phane Siohan. Maeneo ya usambazaji wa umeme ya mji mkuu ndiyo ambayo yalilengwa. Mabaki ya ndege zilizangudondoshwa yalianguka kwenye majengo ya utawala na makazi magharibi mwa mji mkuu wa Ukraine, bila kusababisha hasara yoyote, kulingana na utawala wa kijeshi wa Kyiv.

Shambulio kuu la awali la Urusi lililolenga maeneo ya nishati kote nchini lilianza Desemba 5.

Mashambulizi haya mapya yanakuja wakati msemaji wa Kremlin Dimitri Peskov amehakikishia Jumatano asubuhi kwamba mapigano yanapaswa kudumu kati ya siku ya Krismasi na Siku ya Mwaka Mpya. "Hakuna pendekezo lililotolewa na mtu yeyote, suala hili haliko kwenye ajenda," msemaji wa ofisi ya rais wa Urusi amewaambia waandishi wa habari, ambaye pia alikataa kuweka wazi Tarehe ya hotuba ya kila mwaka ya Vladimir Putin kwa mabunge yote mawili ya Urusi. Hotuba iliahirishwa kwa muda usiojulikana wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.