Pata taarifa kuu

Ukraine: Watoto milioni 7 wanatishiwa na uharibifu wa miundombinu ya nishati, UNICEF yaonya

Mashambulizi ya Urusi inayolenga miundombinu ya nishati ya Ukraine inaleta hatari zinazoongezeka kwa "karibu watoto wote nchini Ukraine - karibu watoto milioni saba" huku halijoto ya majira ya baridi ikiendelea kushuka nchini humo, UNICEF imeonya.

Mapigano yanaendelea kuathiri watoto Ukraine, hasa katika mji mkuu wa Kyiv.
Mapigano yanaendelea kuathiri watoto Ukraine, hasa katika mji mkuu wa Kyiv. REUTERS - RADOVAN STOKLASA
Matangazo ya kibiashara

Bila upatikanaji thabiti wa umeme, joto au maji, "watoto sio tu wanakabiliwa na baridi kali (joto la majira ya baridi linaweza kushuka chini ya -20 ° C) lakini pia hawawezi kufurahia fursa za kujifunza mtandaoni ambazo ni njia pekee ya kupata elimu kwa watoto wengi, huku shule nyingi zikiharibika au kuharibiwa,” Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limebaini katika taarifa.

Kwa kuongezea, vituo vya afya vinaweza kushindwa kutoa huduma muhimu, na mifumo mibovu ya usambazaji wa maji huongeza hatari kubwa zaidi za nimonia, mafua ya msimu, magonjwa yatokanayo na maji na UVIKO-19, linaongeza shirika hilo. Na "zaidi ya tishio la haraka linalotokana na hali ya baridi, watoto pia wananyimwa fursa ya kujifunza au kukaa na uhusiano na marafiki na familia, wakiweka afya zao za kimwili na kiakili katika hatari kubwa" , pia ameelezea wasiwasi wake mkurugenzi mkuu wa UNICEF, ​​​​CatherineRussell, akinukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.