Pata taarifa kuu

Ukraine haina maji na umeme baada ya mashambulizi ya Urusi

Kwa siku ya pili mfululizo, jeshi la Urusi linaendelea na operesheni yake ya mashambulizi ya angani nchini Ukraine. Jumanne hii asubuhi, miundombinu kadhaa muhimu ilikumbwa na mashambulizi - jeshi la Urusi limethibitisha mashambulizi haya - na watu wawili wameuawa. Volodymyr Zelensky amebaini kwamba "umeme umekata kote nchini".

Uharibifu mkubwa uliosababishwa na mashambulizi ya angani ya Urusi hali ambayo imesababisha kukata kwa umeme na gesi nchini Ukraine, huko Korobochkyne, Oktoba 17, 2022.
Uharibifu mkubwa uliosababishwa na mashambulizi ya angani ya Urusi hali ambayo imesababisha kukata kwa umeme na gesi nchini Ukraine, huko Korobochkyne, Oktoba 17, 2022. REUTERS - CLODAGH KILCOYNE
Matangazo ya kibiashara

Katika kipindi cha saa 24 zilizopita, jeshi la Urusi lilishambulia zaidi ya maeneo 35 kwa makombora ya ya masafa ya kati na kutumia ndege zisizo kuwa na rubani ziitwazo Shahed, zilizotengenezwa nchini Iran. Urusi imekuwa ikilenga miundombinu ya nishati.

Wakati majira ya baridi yakipokaribia, Urusi imeharibu 30% ya vinu vya kuzalisha umeme vya Ukraine: haya ni matokeo ya operesheni ya mashambulizui ya angani iliyoanza Oktoba 10, kulingana na kauli ya rais wa Ukraine kwenye Twitter.

Mjini Kyiv, shirika la la umma la DTEK linaripoti "usumbufu" katika usambazaji wa umeme na maji kwa wakazi wa baadhi ya maeneo. Meya, Vitaly Klichko ametoa wito kwa wakazi wa mji mkuu kutunza Β umeme na kuhifadhi maji ya kunywa.

Hakuna umeme au maji huko Zhytomyr, magharibi mwa Kyiv. "Hospitali zinaendeshwa kwa umeme mbadala wa dharura," amesema Meya Sergiy Sukhomlin kwenye Facebook.

Katika eneo la Mashariki, jiji kuu la Dnipro, limeshuhudia makombora mawili ya Urusi yakipiga "miundombinu ya nishati" na kusababisha "moto na uharibifu mkubwa". Sehemu kadhaa za jiji hazina umeme. Upungufu wa umeme na maji pia unaripotiwa huko Pavlograd.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.