Pata taarifa kuu

Wakazi wa jimbo la Kherson watakiwa kukimbilia Urusi kufuatia mshambulizi ya Ukraine

Kiongozi wa Urusi aliyeteuliwa kusimamia jimbo la Kherson nchini Ukraine, Vladimir Saldo, amewataka raia katika eneo hilo kuondoka kufuatia ongezeko la mashambulio kutoka kwa jeshi la Ukraine.

Kutoka Vladimir Saldo kushoto, mkuu wa jimbo la Kherson aliyeteuliwa na Mosco , Yevgeny Balitsky mkuu jimbo la Zaporizhzhia aliyeteuliwa na Moscow, Rais wa Urusi Vladimir Putin, katikati, Denis Pushilin, kiongozi wa jimbo lililojitangaza Jamhuri ya Watu wa Donetsk na Leonid Pasechnik, kiongozi wa waeneo lililojitangaza Jamhuri ya Watu wa Luhansk wakipiga picha wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya majimbo manne ya Ukraine kujiunga na Urusi, katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Ijumaa, Septemba 30, 2022.
Kutoka Vladimir Saldo kushoto, mkuu wa jimbo la Kherson aliyeteuliwa na Mosco , Yevgeny Balitsky mkuu jimbo la Zaporizhzhia aliyeteuliwa na Moscow, Rais wa Urusi Vladimir Putin, katikati, Denis Pushilin, kiongozi wa jimbo lililojitangaza Jamhuri ya Watu wa Donetsk na Leonid Pasechnik, kiongozi wa waeneo lililojitangaza Jamhuri ya Watu wa Luhansk wakipiga picha wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya majimbo manne ya Ukraine kujiunga na Urusi, katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Ijumaa, Septemba 30, 2022. AP - Grigory Sysoyev
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo amewataka wakaazi wa jimbo hilo kujiokoa kwa kukimbilia nchini Urusi, kwenda kupumzika na kusoma, huku akiomba msaada wa Urusi kuwaondoa watu hao. 

Kauli hii imeungwa mkono na Naibu Waziri Mkuu wa Urusi, Marat Khusnullin kupitia taarifa kupitia Televisheni ya taifa. 

Ripoti zinasema kundi la Kwanza la wakaazi wa jimbo hilo, wanatarajiwa kuwasili katika jimbo la Rostov upande wa Urusi siku ya Ijumaa. 

Wanajeshi wa Ukraine wanaendeleza mapamban kuchukua maeneo yaliyotanagzwa na Urusi kuwa ni aradhi take, na tayari wamedhibiti maeno ya Kaskazini Magharibi mwa Kherson. 

Ukraine inasema, katika operesheni zake haiwalengi raia wa kawaida kama inavyoshtumiwa na Urusi. 

Mbali na Kherson, baada ya kuandaa kura ya maoni, Urusi sasa inadai majimbo mengine ya Zaporizhzhia ,Donetsk na  Luhansk ni maeneo yake, hatua ambayo imepingwa na Umoja wa Mataifa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.