Pata taarifa kuu

Putin amhakikishia Modi kwamba anataka kumaliza vita vya Ukraine 'haraka iwezekanavyo'

Viongozi wa Urusi na India wmekutana kwenye mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Rais wa Urusi Vladimir Putin amemhakikishia Waziri Mkuu wa India Narendra Modi Ijumaa hii, Septemba 16 kwamba anataka kumaliza mzozo wa Ukraine "haraka iwezekanavyo", huku akisema kwamba anaelewa "wasiwasi" wa India kuhusu suala hili.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi huko Samarkand, Uzbekistan Septemba 16, 2022.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi huko Samarkand, Uzbekistan Septemba 16, 2022. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

"Ninajua msimamo wako kuhusu mzozo wa Ukraine, wasiwasi wako (...) Tutafanya kilio chini ya uwezo wetu kumaliza kila kitu haraka iwezekanavyo," Vladimir Putin amesema wakati wa mazungumzo na Narendra Modi.

"Mheshimiwa, naelewa kuwa huu sio wakati wa vita," Narendra Modi pia amemwambia Vladimir Putin huko Samarkand, kando ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) nchini Uzbekistan, kulingana na picha za televisheni. Ni mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana tangu uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Lakini Narendra Modi hata hivyo amesisitiza umuhimu wa "demokrasia, diplomasia na mazungumzo". Viongozi hao wawili watajadili "jinsi ya kusonga mbele kwa njia ya amani", ameongeza Waziri Mkuu wa India.

India imejiepusha na kukemea kwa uwazi uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ambao umesababisha kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa nyinginezo. New Delhi inaitolea wito Moscow "nguzo muhimu" ya sera ya kigeni ya India kwa sababu ya "ushirikiano wake wa kimkakati" kwa usalama wake wa kitaifa. Matamshi ya kiongozi huyo wa India yamekuja siku moja tu baada ya Vladimir Putin kukiri kwamba China, mshirika mkuu wa Urusi, ina "wasiwasi" kuhusu mzozo wa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.