Pata taarifa kuu

Ukraine: Makaburi zaidi ya 450 yagunduliwa karibu na Izium

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ambaye alitembelea Izium siku ya Jumatano na kudai kwamba kaburi la halaiki limegunduliwa katika jiji hili la kaskazini mashariki mwa Ukraine, ambalo lilichukuliwa kutoka kwa wanajshi wa Urusi siku chache zilizopita. Kulingana na Kyiv, makaburi 450 yalipatikana msituni.

Oleg Kotenko, kamishna wa masuala yanayohusiana na watu waliopotea katika mazingira tatanishi, anapiga picha kaburi katika mki wa Izium, Alhamisi, Septemba 15, 2022.
Oleg Kotenko, kamishna wa masuala yanayohusiana na watu waliopotea katika mazingira tatanishi, anapiga picha kaburi katika mki wa Izium, Alhamisi, Septemba 15, 2022. AP - Evgeniy Maloletka
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake kupitia televisheni usiku wa kuamkia leo Rais Volodymyr Zelensky amesema eneo hilo limebainika karibu na mji wa Izium katika mkoa wa Kharkiv.

Kwa sasa hakuna taarifa zaidi kuhusiana na makaburi hayo, lakini yote hayo yalifahalika kupitia picha chache tu zilizovuja Alhamisi jioni. Inafahamika tu kwamba kuna kaburi kwenye ukingo wa jiji, katika msitu, ambalo lilipatikana wakati wa ukombozi wa Izium. Makaburi kadhaa yamepangwa na majina ya watu, utambulisho, tna arehe za kuzaliwa. Lakini haijulikani kwa sasa ikiwa makaburi haya yana miili ya wanajeshi ambao waliuawa wakati wa shambulio la mji huo miezi sita iliyopita au raia ambao waliuawa wakati wa uvamizi wa Urusi. Bado hakujapatikana zaidi taarifa kuhusu wasifu na utambulisho wa watu hawa.

"Bucha, Mariupol, na sasa, kwa bahati mbaya, Izium," rais wa Ukraine alisema Alhamisi jioni, Septemba 15, katika ujumbe wake wa kila siku wa video.

Makaburi mia nne na hamsini

Lakini Volodymyr Zelensky alitaja neno "kaburi la watu wengi", neno lenye nguvu sana. Wanahabari wa Ukraine na wa kimataifa watasafiri Ijumaa hii kwenda Izium. "Makaburi mia nne na hamsini" yaligunduliwa karibu na Izium, mji wa mashariki mwa Ukraine uliotekwa tena hivi karibuni kutoka mikononi mwa vikosi vya Urusi, mshauri wa rais Mykhaïlo Podoliak amesema leo Ijumaa.

Serikali ya Kyiv imekuwa ikiishutumu Urusi kwa kufanya mashambulizi dhidi ya raia kwa uwezekano wa uhalifu wa kivita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.