Pata taarifa kuu

Zelensky azuru maeneo yaliokombolewa na jeshi lake

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametembelea mji wa Izyum, uliochukuluwa na vikosi vyake katika mapambano dhidi ya Urusi, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. 

Rais Volodymyr Zelensky katika picha iliyotolewa na idara ya vyombo vya habari vya rais wa Ukraine Julai 23, 2022.
Rais Volodymyr Zelensky katika picha iliyotolewa na idara ya vyombo vya habari vya rais wa Ukraine Julai 23, 2022. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Rais Zelensky katika ziara yake, amekutana na wanajeshi wa nchi yake na kuwapongeza kwa kuwashinda wanajeshi wa Urusi katika mji huo. 

Wakati wa ziara hiyo, bendera ta Ukraine ilipandishwa tena huku kiongozi wa nchi hiyo akisema bendera hiyo itapandishwa katika miji yote na vijiji kote nchini humo. 

Baada ya ushindi huo, wanajeshi wa Ukraine wanasema kwa sasa wanalenga kuikomboa miji katika jimbo la Donbas ambalo linadhibitiwa na wanajeshi wa Urusi. 

Wiki iliyopita, rais Zelesky alisema wanajeshi wa Ukraine walikuwa wamechukua tena êneo la ardhi lenye ukubwa wa mradi Kilomitra 1000 na sasa imefikia Elfu tatu. 

Rais Joe Biden wa Marekani ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kuipa Ukraine msaada wa fedha kununua silaha za kivita, ameisifu nchi hiyo kwa kupiga hatua katika kuchukua maeneo yanayoshikiliwa na jeshi la Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.