Pata taarifa kuu
VITA-DIPLOMASIA

Ukraine: Mawaziri wa ulinzi wa Marekani na washirika wake kukutana Septemba 8

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin atawapokea mawaziri wenzake kutoka nchi washirika nchini Ujerumani Septemba 8 kuandaa msaada wa kijeshi kwa Ukraine dhidi ya Urusi.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin REUTERS - KAI PFAFFENBACH
Matangazo ya kibiashara

Lloyd Austin "tena amewaalika mawaziri wa ulinzi na maafisa wakuu wa kijeshi kutoka kote ulimwenguni kujadili mzozo wa sasa wa Ukraine na changamoto mbalimbali za usalama zinazowakabili washirika wa Marekani," taarifa ya wizar ya Ulinzi ya Marekani.

Hayo yanajiri wakati Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) ametangaza leo Jumatatu asubuhi kwamba ujumbe wa shirika hilo uko njiani kuelekea kwenye kinu cha nyuklia cha Zaporizhia nchini Ukraine, kilicholengwa na mashambulizi katika wiki za hivi karibuni, hali iliyotia hofu ya kutokea kwa ajali kubwa

"Siku imewadia, ujumbe wa IAEA kwenda Zaporizhia sasa uko njiani. Ni lazima tulinde usalama wa Ukraine na mtambo mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme barani Ulaya”, ameandika Rafael Grossi kwenye Twitter, akibainisha kuwa ujumbe huo utawasili kwenye eneo hilo"baadaye wiki hii". Katika picha iliyoambatana na ujumbe wake, mkuu wa IAEA akiwa katika picha ya pamoja na timu ya watu kumi, wakiwa wamevalia kofia na fulana zenye nembo ya shirika la Umoja wa Mataifa.

Rafael Grossi alikuwa ameomba kwa miezi kadhaa kuweza kwenda kwenye eneo la tukio, akionya juu ya "hatari halisi ya maafa ya nyuklia". Kiwanda cha Zaporizhia, ambapo kunapatikana vinu sita kati ya 15 vya Ukraine, kilidhibitiwa na wanajeshi wa Urusi mapema mwezi Machi, muda mfupi baada ya uvamizi dhidi ya Ukraine kuanza mnamo Februari 24, na kiko karibu na uwanja wa mapigano kusini mwa Ukraine.

Kyiv na Moscow wanatuhumiana kila mmoja kwa kufanya mashambulizi karibu na kituo hiki cha nyuklia, karibu na mji wa Energodar, kwenye Mto Dnieper, na hivyo kuweka kinu hiki katika hatari. Siku ya Jumamosi shirika la taifa la nishati ya nyuklia la Ukraine, Energoatom, lilionya juu ya hatari ya uvujaji wa mionzi na moto baada ya mashambuizi mapya. Katika wiki za hivi majuzi, nchi za magharibi zilitiwa wasiwasi na hali inayojiri karibu na kinu cha Zaporijgia. Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kukomeshwa kwa shughuli zote za kijeshi katika eneo lililokaribu na kituo hiki cha nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.