Pata taarifa kuu
Sri Lanka - Siasa

Sri Lanka: Kaimu rais Ranil Wickremesinghe apishwa

Waziri mkuu wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe, ameapishwa kuhudumu kama rais, wakati huu wandamanaji wakiendelea kuandamana wakilalamikia kudorora kwa uchumi na kumtaka, Ranil pia ajiuzulu.

Waziri Mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe akiapishwa kama rais wa muda, Colombo, Julai 15, 2022
Waziri Mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe akiapishwa kama rais wa muda, Colombo, Julai 15, 2022 AP
Matangazo ya kibiashara

Ranil anajaza nafasi ya Gotabaya Rajapaksa, ambaye amekimbilia taifa la Singapore, baada ya wandamanaji kuvamia makaazi yake.

Wandamanaji  wamekuwa wakipuuza hali ya dharura iliotangazwa, ili kusherehekea kujiuzulu kwa Rajapakasa.

Sri Lanka inapitia wakati mugumu wa kiuchumi, wakati huu uhaba wa chakula, mafuta na bidhaa nyingine muhimu pia ukiripotiwa.

Shughuli ya bunge ya kumchagua rais mpya itaanza kesho, wabunge wakitarajiwa kupiga kura juma lijalo kumchagua rais.

Kutokana na hali ya kwamba  wabunge wengi ni wa chama tawala, huenda wakamchagua Wickremesinghe , ambaye ana uhusiano wa karibu na familia ya Rajapaksa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.