Pata taarifa kuu
Sri Lanka-siasa

Sri Lanka: Hali ya dharura imetangazwa baada ya rais kutoroka.

Hali ya dharura imetangazawa nchini Sri Lanka saa chache tu baada ya rais Gotabaya Rajapaksa kutoroka kwenye taifa hilo linaloshuhudia mzozo wa kiuchumi, imesema taarifa ya ofisi ya waziri mkuu.

Wandamanaji wakikabiliana na polisi jijini Colombo nchi Sri Lanka.
Wandamanaji wakikabiliana na polisi jijini Colombo nchi Sri Lanka. REUTERS - DINUKA LIYANAWATTE
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa waziri mkuu Ranil Wickremesinghe, Dinouk Colombage, katika taarifa yake anaeleza kuwa hatua hii imechukuliwa kama njia moja ya kabiliana na kinachoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Raia wa mkoa wa magharibi unaojumuisha jiji kuu la Colombo wametakiwa kutotembea nje polisi ikieleza kuwa hatua hii imechukuliwa ilikabiliana na idadi kubwa ya wandamanaji wanaoendelea kujitokeza baada ya Rajapaksa kutorokea visiwani Maldives kwa usaidizi wa jeshi.

Polisi wamewatawanya maelfu ya wandamanaji waliokuwa wamepiga kambi nje ya ofisi ya waziri mkuu wakimtaka ajiuzulu.Polisi ikisema kuwa wameagizwa kuwatwanya wandamanaji wanaovuruga mipangilio ya nchi.

Siku ya jumamosi, maelfu ya wandamanaji waliwazidi nguvu walinzi katika makao rasimi ya rais Rajapaksa akilazimika kutorokea katika kambi ya jeshi na kisha baadae kuondoka nchini humo.

Taarifa zinasema kuwa huenda rais huyo akatangaza kujiuzulu jumatano atakapofika katika nchi ya tatu .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.