Pata taarifa kuu

Urusi yafunga ofisi ya Deutsche Welle, baada ya kituo cha RT kuwekewa marufuku Ujerumani

Urusi imeagiza Alhamisi hii, Februari 3, kufungwa kwa ofisi ya kituo cha redio na televisheni cha kimataifa cha Ujerumani Deutsche Welle nchini humo, ili kulipiza kisasi kupigwa marufuku kwa kituo cha  habari cha Urusi cha RT kutangaza nchini Ujerumani.

Hatua zilizotangazwa na Moscow pia zinahusisha "kufutwa kwa kibali cha wafanyakazi wote" kutoka kwa ofisi ya idhaa ya Kirusi ya Deutsche Welle.
Hatua zilizotangazwa na Moscow pia zinahusisha "kufutwa kwa kibali cha wafanyakazi wote" kutoka kwa ofisi ya idhaa ya Kirusi ya Deutsche Welle. AFP - YURI KADOBNOV
Matangazo ya kibiashara

Urusi iliapa kulipiza kisasi baada ya kupigwa marufuku kwa kituo cha habari cha Urusi cha RT kwa lugha ya Kijerumani, hatua ambayo haikuchukua muda mrefu. "Hatua ya kulipiza kisasi" inahusisha na "kufungwa kwa ofisi " ya Deutsche Welle nchini Urusi, "kuondolewa kwa kibali cha wafanyakazi wote" kutoka kwa ofisi hii na "kupigwa marufuku " chombo hiki kurusha matangazo yake kwenye ardhi ya Urusi. "

Kulingana na Moscow, vikwazo pia vimepangwa dhidi ya "wawakilishi wa serikali ya Ujerumani na miundo ya umma inayohusika katika kizuizi cha utangazaji wa RT", chombo ambacho inakuza haswa msimamo wa Kremlin nje ya nchi. Mamlaka nchini Urusi imebaini kuwa hatua hizi zilikuwa sehemu ya "hatua za kwanza", na kuahidi majibu ya ziada "kwa wakati unaofaa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.