Pata taarifa kuu
UJERUMANI-USHIRIKIANO

Ukraine: Berlin yaitishia Moscow kufunga bomba la gesi la Nord Stream 2

Bomba jipya la gesi la Ujerumani na Urusi lenye utata la Nord Stream 2 halitaruhusiwa kufanya kazi ikiwa Moscow itaivamia Ukraine, amesema Annalena Baerbock, Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Ujerumani. Wakati huo huo G7 imetishia Urusi kuwa"itakabiliwa na hali ngumu" ikiwa itafanya uchokozi wa kijeshi dhidi ya Kiev.

Bomba la gesi la Nord Stream 2 halitaruhusiwa kufanya kazi katika ikiwa Urudi itaendelea harakati zake za kuivamia Ukraine.
Bomba la gesi la Nord Stream 2 halitaruhusiwa kufanya kazi katika ikiwa Urudi itaendelea harakati zake za kuivamia Ukraine. Odd ANDERSEN AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali ya wasiwasi ya usalama, "ilikubaliwa kati ya Wamarekani na serikali ya zamani ya Ujerumani" ya Angela Merkel "kwamba ikiwa Uusi itaendelea harakati zake za kuivamia Ukraine, bomba hili haliwezi kutumika", ametangaza Annalena Baerbock, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani. Nchi za Magharibi zimeishutumu Urusi kwa wiki chache kwa kujiandaa kwa uwezekano wa kuivamia Ukraine, licha ya kukanushwa na Ikulu ya Kremlin.

Bomba hili la gesi, linaloungwa mkono kwa dhati na Vladimir Putin na Angela Merkel, linashutumiwa na nchi nyingi. Marekani na nchi kadhaa za Ulaya Mashariki, kuanzia Poland, zina wasiwasi kwamba Ulaya inategemea sana Urusi ya Putin.

Hata hivyo, Ukraine, hadi sasa moja ya nchi kuu za usafirishaji wa gesi ya Urusi kwenda Ulaya, inaogopa kulipia mradi huu ambao hhaina manufaa nao na kudhoofika kiuchumi na kidiplomasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.