Pata taarifa kuu
URUSI-DIPLOMASIA

Nord Stream 2: mradi wa bomba la gesi watishiwa na mvutano kati ya Urusi na Ukraine

Mikutano ya Marekani na Urusi, mkutano kati ya NATO na Urusi, mkutano wa shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya, lenye makao yake mjini Vienna, tangu Januari 10, mikutano ya kidiplomasia imekuwa ikifanyika kwa kuokoa mvutano kati ya mataifa hayo mawili.

Ikiwa Moscow itafanya uvamizi dhidi ya Ukraine, vikwazo dhidi ya mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2 kati ya Urusi na Ujerumani vitazingatiwa.
Ikiwa Moscow itafanya uvamizi dhidi ya Ukraine, vikwazo dhidi ya mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2 kati ya Urusi na Ujerumani vitazingatiwa. Odd ANDERSEN/AFP
Matangazo ya kibiashara

Suala kubwa hapa ni hofu ya uvamizi wa Moscow dhidi ya Ukraine, ambapo Urusi inatishiwa kulipizwa kisasi ikiwa operesheni kama hiyo itaamuliwa.

Miongoni mwa hatua zinazowezekana ni vikwazo dhidi ya mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2 kati ya Urusi na Ujerumani. Suala ambalo linasababisha mgawanyiko ndani ya muungano mpya ulio madarakani mjini Berlin.

"Hatupaswi kuingiza mradi wabomba la Nord Stream 2 kwenye mzozo huu," Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Christine Lambrecht amesema. Yeye, kama viongozi wengine kutoka vyama vinavyounda muungano katika serikali ya Ujerumani, amesisitiza kuwa chama chake hakitaki mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2, kuathiriwa na uwezekano wa vikwazo ambavyo vitaikumba Moscow kama itathubutu kuivamia Ukraine.

Bomba la gesi linachukuliwa kuwa mradi wa kibinafsi na sio wa kijiografia. Hili lilisisitizwa hivi karibuni na mkuu mpya wa serikali Olaf Scholz, na hivyo kupunguza kauli za awali za kutishia Urusi na athari ya bomba la gesi katika kama itafanya uvamizi dhidi ya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.