Pata taarifa kuu

Ukraine: EU yataka kuzindua mazungumzo na Moscow ili kuepuka mvutano wa kidiplomasia

Katika hali inayoendelea Ukraine, sauti kadhaa muhimu zinasikika juu ya hali ya hatari na wakati mwingine ya kutia uoga ya Umoja wa Mataifa, ambayo iliamua kuwaondoa wafanyakazi kwenye ubalozi wake huko Kiev, wakati hali ya usalama nchini Ukraine haijaamua hivo.

Wanajeshi wa Urusi wakifanya mazoezi ya kufyatua risasi huko Kadamovskiy katika mkoa wa Rostov, kusini mwa Urusi, Januari 13, 2022.
Wanajeshi wa Urusi wakifanya mazoezi ya kufyatua risasi huko Kadamovskiy katika mkoa wa Rostov, kusini mwa Urusi, Januari 13, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Jioni ya Jumanne, Januari 25, ndege ya mizigo ya Marekani ilitua Kiev, ikitoa dazeni kadhaa za makombora ya kukinga vifaru vya aina ya Mkuki kwa jeshi la Ukraine. Katika muktadha huu, nchi za Umoja wa Ulaya, na hususan Ufaransa, wanajaribu kujitengenezea nafasi katika mchakato wa kuondoa hali ya mzozo kati ya Marekani na Urusi, na Emmanuel Macron atajaribu kukutana tena kwa mazungumzo na Vladimir Putin na kuanza tena mazungumzo katika "mfumo wa Normandy", ameripoti mwandishi wetu huko Kiev, Stéphane Siohan.

Jumatano hii, majadiliano katika muundo wa Normandy yatafanyika mjini Paris katika ngazi ya washauri wa kisiasa kutoka Urusi, Ukraine, Ufaransa na Ujerumani.

Pia siku ya Jumanne, katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari mjini Berlin na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Emmanuel Macron alitangaza kuwa atakuwa na mazungumzo ya simu Ijumaa Januari 28 na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Emmanuel Macron na Olaf Scholz katika mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari mjini Berlin, hata hivyo walisihi kuendelea kwa mazungumzo na Moscow na kukaribisha mikutano mingi ya kidiplomasia ya siku chache zilizopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.