Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron na Olaf Scholz kuijadili hali nchini Ukraine

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz wanakutana jijini Berlin kujadiliana kuhusu uwezekano wa Urusi kuishambulia Ukraine, katika mkutano ambao viongozi hao wanatarajiwa kuwa na msimamo mmoja.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuonyesha msimamo wake kuhusu uwezekano wa Urusi kuishambulia Ukraine.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuonyesha msimamo wake kuhusu uwezekano wa Urusi kuishambulia Ukraine. AP - Jean-Francois Badias
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yanakuja siku moja, baada ya Marekani kusema wanajeshi wake zaidi ya Elfu nane, yapo tayari kwenda Mashariki mwa Ulaya, kuilinda Ukraine, iwapo itashambuliwa na Urusi.

Naye Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amewaambia wabunge kuwa, Uingereza, Marekani na mataifa mengine ya Magharibi yamekubaliana kujibu kwa pamoja iwapo Urusi itaishambulia Ukraine.

Zaidi ya wanajeshi Laki Moja wa Urusi wameendelea kufanya mazoezi karibu na mpaka wa Ukraine, huku kukiwa na wasiwasi kuwa inaweza kuishambulia nchi hiyi jirani.

Wakati Urusi ikiishtumu Marekani kwa kuchochea mzozo kati ya Ukraine kwa kuwa tayari kuongeza kiwango cha wanajeshi wake kwa muungano wa NATO, Washington na mataifa ya Magharib yameapa kusimama na Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.