Pata taarifa kuu

Ukraine: Emmanuel Macron na Olaf Scholz kuwa kitu kimoja dhidi ya Urusi

Rias wa Ufaransa Emmanuel Macron ziarani nchini Ujerumani pamoja na mwenyeji wake Olaf Scholz walisisitiza Jumanne mshikamano wao na Kiev na azimio lao dhidi ya Moscow, huku wakitumai kuwa mazungumzo na Urusi yanaweza kusaidia kusitisha uhasama.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Januari 25, 2022 huko Berlin.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Januari 25, 2022 huko Berlin. AP - Tobias Schwarz
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya kwanza ya Emmanuel Macron mjini Berlin tangu kuchaguliwa kwa Kansela mpya Olaf Scholz ilijikita zaidi katika mvutano kati ya Ukraine na Urusi. Ili kuonyesha umoja wao na msimamo wao dhidi ya Urusi kama Moscow itaivamia Ukraine, viongozi hao wawili walitumia maneno sawa, wakisema Urusi" itakiona cha mtema kuni".

Zaidi ya mzozo wa sasa, rais wa Ufaransa ameshutumu sera ya Vladimir Putin ya kuvuruga utulivu katika maeneo ya zamani ya muungano wa Sovieti ya zamani, ameripoti mwandishi wetu huko Berlin, Pascal Thibaut. "Hali ambayo tunajikuta leo inahitaji maandalizi ya majibu ya pamoja ambayo yakabiliana na mpango wa Urusi", alitangaza.

Emmanuel Macron na Olaf Scholz hata hivyo walisihi kuendelea kwa mazungumzo na Moscow na kukaribisha mikutano mingi ya kidiplomasia ya siku chache zilizopita. Jumatano hii, majadiliano katika muundo wa Normandi yatafanyika mjini Paris katika ngazi ya washauri wa kisiasa kutoka Urusi, Ukraine, Ufaransa na Ujerumani. Siku ya Ijumaa, Emmanuel Macron atamuomba mwenzake Putin "ufafanuzi" wakati wa mahojiano ya simu.

Scholz anajitetea

"Tunahitaji kuzungumza. Tunabishana lakini inabidi tujaribu kusonga mbele na kutoka katika hali hii tete. Nimeridhishwa na uongozi tunaouona hivi sasa”, alibaini Kansela wa Ujerumani. "Kwa hivyo tunatarajia Urusi kuchukua hatua za wazi kuchangia katika kuzorota kwa hali hiyo na sote tunakubali kwamba uvamizi wa kijeshi ungekuwa na madhara makubwa," hata hivyo alionya.

Alipoulizwa kuhusu kukataa kwa Ujerumani, ambayo ilikosolewa na nchi nyingine, kupeleka silaha kwa Ukraine wakati nchi kadhaa za Ulaya zinakusudia kufanya hivyo, Olaf Scholz alijitetea: "Serikali ya Ujerumani imekuwa ikikataa katika miaka ya hivi karibuni utoaji wa silaha hatari, lakini tumefanya mengi kusaidia uchumi na demokrasia nchini Ukraine. »

Kwa upana zaidi, Ujerumani inakosolewa na nchi nyingine kwa msimamo unaoonekana kuwa kulegalega kuhusu Moscow. Kwa upande wa Gazeti la kila siku la Tagesspiegel, nia ya Emmanuel Macron na Olaf Scholz ya kuendelea na mazungumzo na Urusi inawaleta pamoja wwawili hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.