Pata taarifa kuu
JAPANI-AFYA

Corona: Japan kuongeza muda wa hali ya hatari ya kiafya

Serikali ya Japani imepanga kutangaza hali ya hatari ya kiafya katika wilaya tatu jirani za Tokyo na ile ya Osaka, kusini mwa nchi hiyo, kukabiliana na kuibuka tena kwa visa vya maambukizi ya virusi vya Corona, shirika la habari la Kyodo limeripoti.

Mji mkuu wa Japani, mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki, tayari uko chini ya vizuizi tangu Julai 12  hadi Agosti 22. Hali ya hatari inabaini kwamba migahawa inatakiwa kufungwa mapema na huacha kutoa huduma ya pombe.
Mji mkuu wa Japani, mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki, tayari uko chini ya vizuizi tangu Julai 12 hadi Agosti 22. Hali ya hatari inabaini kwamba migahawa inatakiwa kufungwa mapema na huacha kutoa huduma ya pombe. Yasuyoshi CHIBA AFP
Matangazo ya kibiashara

Maamuzi yatatangazwa Ijumaa wiki hii, Waziri Mkuu Yoshihide Suga amesema.

Kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa janga hilo, idadi ya kila siku ya maambukizi ya SARS-CoV-2 imezidi kizingiti cha watu10,000 siku ya Alhamisi, kulingana na vyombo vya habari vya Japani.

Halmashaui ya manispaa ya mji wa Tokyo imetangaza rekodi ya maambukizi 3,865 katika muda wa saa 24, dhidi ya 3,177 siku moja kabla.

Mji mkuu wa Japani, mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki, tayari uko chini ya vizuizi tangu Julai 12  hadi Agosti 22. Hali ya hatari inabaini kwamba migahawa inatakiwa kufungwa mapema na huacha kutoa huduma ya pombe.

Kulingana na NHK, muda wa hali ya hatari utaongezwa hadi Agosti 31.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.