Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-JAPAN

Japan kuondoa hali ya hatari kuelekea michezo ya Olimpiki

Serikali ya Japan itaondoa hali ya hatari iliyotangazwa  tarehe 20 mwezi Juni mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki itayofanyika jijini Tokyo kuanzia tarehe 23 mwezi Julai.

Nembo ya michezo ya Olimpiki
Nembo ya michezo ya Olimpiki Behrouz MEHRI AFP
Matangazo ya kibiashara

Jiji la Tokyo na maeneo mengine ya nchi hiyo, yamekuwa chini ya hali hiyo ya hatari tangu tarehe 25 Aprili kutokana na ongezeko la visa vya maambukizi ya corona.

Kuelekea michezo hii, serikali nchini humo imetangaza kuwa itawaruhusu mashabiki 10,000 kushuhudia michezo hiyo lakini wale kutoka nje ya nchi hawataruhusiwa kutokana na janga la Corona.

Waandalizi wa mashindano haya wanasema asilimia 80 watapewa chanjo kabla ya kushiriki kwenye michezo hiyo na hawataruhisiwa kutangamana na wananchi wa Japan.

Michezo hii ilitarajiwa kufanyika mwaka 2020, laini ikaahirishwa kwa sababu ya janga la corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.