Pata taarifa kuu
JAPAN-AFYA

Hali ya dharura yaongezwa Japani kabla ya Michezo ya Olimpiki

Japani imeamua kuongeza muda wa hali ya dharura katika maeneo tisa, ikiwa ni pamoja na mji wa Tokyo, kwa wiki tatu kuanzia Ijumaa hii, wakati janga la COVID-19 linaonekana kushika kasi ndani ya kipindi cha miezi miwili kabla ya kufunguliwa Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto katika mji mkuu wa Japan.

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga akiinama mbele ya bendera ya kitaifa katika mkutano na waandishi wa habari, katika makaazi rasmi ya waziri mkuu huko Tokyo, baada ya uamuzi wa serikali wa kuongeza muda wa hali ya dharura wakati COVID-19 ikishika kasi, Japan Mei 28, 2021.
Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga akiinama mbele ya bendera ya kitaifa katika mkutano na waandishi wa habari, katika makaazi rasmi ya waziri mkuu huko Tokyo, baada ya uamuzi wa serikali wa kuongeza muda wa hali ya dharura wakati COVID-19 ikishika kasi, Japan Mei 28, 2021. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Wakati mgogoro wa kiafya ukiendelea kukabili mfumo wa afya wa Japan, Waziri Mkuu Yoshihide Suga ametangaza kuongeza muda wa hali ya dharura hadi Juni 20. awali ilitangazwa kuwa hali ya dharura itaondolewa Mei 31.

Licha ya kupungua kwa maambukizi mapya, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 waliolazwa hospitalini imefikia viwango vya rekodi katika siku za hivi karibuni nchini Japani.

Maendeleo dhaifu ya kampeni ya chanjo katika nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na wasiwasi juu ya kuibuka kwa ainai mpya ya kirusi cha Corona cha SARS-CoV-2, imeongeza maandamano dhidi ya Michezo hiyo, madaktari kadhaa, viongozi kadhaa wa kampuni lakini pia mamia ya maelfu ya raia walitaka ifutwe.

Mamlaka ya Japani, Kamati ya Kuandaa Michezo na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) inahakikisha kuwa hatua kali za kuzuia janaga hilo zitachukuliwa wakati wa Michezo ya Tokyo, ambayo iliahirishwa mwaka jana kwa sababu ya janga hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.