Pata taarifa kuu
JAPANI-AFYA

Coronavirus: Japani kuidhinisha chanjo zaidi

Japani inatarajia kuidhinisha utumiaji wa chanjo za COVID-19 zilizotengenezwa na maabara ya Moderna na AstraZeneca baada ya kupata idhini kutoka kwa mamlaka ya afya siku moja kabla.

Japani imejitahidi kununua dozi milioni 120 za chanjo hiyo, ikiwa inatosha kutoa chanjo kwa watu milioni 60.
Japani imejitahidi kununua dozi milioni 120 za chanjo hiyo, ikiwa inatosha kutoa chanjo kwa watu milioni 60. REUTERS - KIM KYUNG-HOON
Matangazo ya kibiashara

Japani ilizindua kampeni yake ya chanjo katikati ya mwezi Februari ikitumia chanjo ya Pfizer, lakini hadi sasa imechanja asilimia 3.9 tu ya raia wake.

Vyombo vya habari vimeripoti leo Ijumaa kuwa licha ya idhini inayotarajiwa ya chanjo mbili za ziada, serikali ilikuwa inatarajia kusubiri kabla ya kutumia chanjo ya AstraZeneca, kwa sababu ya wasiwasi juu ya hatari uwezekano wa kuganda kwa damu.

Japani imejitahidi kununua dozi milioni 120 za chanjo hiyo, ikiwa inatosha kutoa chanjo kwa watu milioni 60.

Tofauti na nchi zingine za Kundi llinaloundwa na nchi Saba (G7) ambazo zimeanza kufuta hatua za kuwataka raia kutotembea kutokana na Corona, sehemu kubwa ya Japani inabaki chini ya hatua za dharura kama sehemu ya kudhibiti mlipuko wa nne wa janga hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.