Pata taarifa kuu
JAPAN-AFYA

Coronavirus: Japan yapanga kusambaza chanjo ya AstraZeneca kwa Taiwan

Japan imetangaza kwamba inajianda kuchangia na nchi zingine chanjo dhidi ya COVID-19, baada ya kamati ya chama tawala kuiomba ipeleke sehemu ya chanjo yake ya AstraZeneca kwa Taiwan.

Japan iliidhinisha chanjo ya AstraZeneca wiki iliyopita na kuahidi kununua dozi milioni 120.
Japan iliidhinisha chanjo ya AstraZeneca wiki iliyopita na kuahidi kununua dozi milioni 120. REUTERS - KIM KYUNG-HOON
Matangazo ya kibiashara

Taiwan inapambana na idadi kubwa ya visa vya maambukizi ya ndani na karibu 1% tu ya raia wake kwa jumla ya zaidi ya milioni 23 wamepewa chanjo hadi sasa.

"Tunaamini ni muhimu kuhakikisha upatikanaji wa usawa wa chanjo salama na madhubuti katika nchi zote na majimbo yote ili kufikia afya kwa wote," msemaji wa serikali Katsunobu Kato, amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Masahisa Sato, mkuu wa kamati ya chama tawala inayohusika na uhusiano na Taiwan, amesema mapema Ijumaa kwamba serikali inapaswa kutoa chanjo kwa Taiwan haraka iwezekanavyo, na kuongeza "wakati Japan ilikuwa katika mahitaji, Taiwan ilitusaidia kwa kututumia barakoa milioni 2. "

Japan iliidhinisha chanjo ya AstraZeneca wiki iliyopita na kuahidi kununua dozi milioni 120. Lakini hakuna mipango ya haraka ya kutumia chanjo nchini humo, kwa sababu ya wasiwasi unaosababishwa juu ya hatari ya kuganda kwa damu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.